Benard Morrison Amerudi Mazoezini Kuikabiri Simba

Benard Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Julai 12, Uwanja wa Taifa.

Morrison alikuwa kwenye mvutano na Yanga kutokana na ishu ya mkataba ambapo kwa sasa inaelezwa kuwa tayari kila kitu kimekamilika kwa mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki kurejea uwanjani.

Alirejea mazoezini Julai 2 akiwa ni mwenye furaha na hajasafiri na timu iliyokwenda Mara ambapo kesho itakuwa na mchezo dhidi ya Biashara United.

Morrison amesema:”Nipo na furaha kurejea ndani ya Yanga na mimi ni mchezaji wa Yanga hivyo nitafanya kazi yangu kwa kuwa ninapenda kucheza kwa furaha.

“Kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba nipo tayari na nikipata nafasi ya kufunga nitafunga kwani kazi ya mchezaji ni kutimiza majukumu yake,” amesema.

Luc Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hatamtumia kwenye mchezo wa Biashara United ila Morrison amemwambia yupo tayari kucheza.

“Masuala yake mengine mimi siwezi kuzungumzia ni juu ya uongozi ila mchezaji ameniambia yupo tayari kucheza kwa ajili ya timu na kwenye mchezo wetu dhidi ya Biashara United sitamtumia,” amesema.

Morrison alifunga kwenye mchezo wake wa kwanza wa dabi mbele ya Simba Uwanja wa Taifa Machi 8 wakati Yanga ikishinda bao 1-0.

47 Komentara

    Swali he atawafunga Tena au watafungwa wao maana Simba wapo Moto sanaa

    Jibu

    Mechi itakuwa Kali Sana hiyo

    Jibu

    Ina pendeza sanaa rudi hafanye kweli mpaka kwenye mech sasa

    Jibu

    Mpira wa Bongo una mambo sana, Haya Yanga bakuli la mshahara wa Morrisson limeshapita??

    Jibu

    Morisson ni mchezaji mzuri Sana! Tania zake Kama balotelli..ila asijidanganye kuwafunga Simba safari hii kazi wanayo#meridianbettz

    Jibu

    Nadhani kurudi kwake sio tishio kwa timu ya simba

    Jibu

    Hana maajabu simba lazima ishinde

    Jibu

    Mashabiki wa yanga hii ni habari nzuri#meridianbettt

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki wa yanga mnyama anarudi tena uwanjani kitawaka siku iyo

    Jibu

    Simba baba lao ataakirudi aitokei Mara mbali.

    Jibu

    Benard Morrison ni mchezaji mzuri sana kwa kiwango chake ataweza kuwafunga simba hata wachezaji wenyewe wanamjua uwezo wake hapo kama namuona manara anavyo wapangia wachezaji wa simba wakamkwatue miguu ili yanga ifungwe ila kwa uwezo wa mwenyezi mungu yanga itashinda

    Jibu

    Asante meridianbet #kwa taarifa

    Jibu

    Simba ndio mkali wao hata akirudi nani hatuogopi tunakiwasha tuu uwanjani

    Jibu

    Itakuwa bonge la mechi simba lazima ichukue ushind#meridianbettz

    Jibu

    Huyo ni mtoto Mdogo sana kwa simba

    Jibu

    Simba lazima washinde na piya wako vizuri

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki wa yanga

    Jibu

    Yanga damu

    Jibu

    Morrison kaz anayo kuikabili wekundu wa msimbazi patakuwa apatoshi hapo

    Jibu

    Hii mechi itakuwa moto

    Jibu

    Hii mechi kabambe

    Jibu

    acheni popoganda mpira dk 90 tusubirini iyo siku tuone mbabe atakua nani

    Jibu

    Hizi drama hazina nafasi ktk ulimwengu wa watu wenye dhamira kutengeneza timu na ligi inayovutia. Haieleweki vema kama masuala yake yametatuliwa au la#meridianbettz

    Jibu

    Huyo Morrison hata Kama amerudi mazoezini wasimuanzishe kwenye kikosi cha kwanza atawafungisha ni mchezaji wa simba Huyo mamluki tu.

    Jibu

    Tusubir iyo siku ifike

    Jibu

    Lazima arudi huyo mchezaji ni wa Yanga sehemu nyingine akienda anaangaika tu

    Jibu

    Morrison kiukweli ni mchezaji mzuri kutokana na masilahi ya timu aliamua kusepa kimia kimia na kusaini mikata na simba sports club ila sio mbaya kwa kubanwa na sheria na kurudi katika klabu yake ya zamani ili kumaliza mkataba wake then anaweza kwenda anapotaka ila kwa upande wa game itakuwa kali maana tunajua kuwa wawili hawa wakikutana inakuwa balaa bonge la dabi

    Jibu

    Maoni:Mpira dk 90 tunasubiri tuone nan ni nani!

    Jibu

    Uyu jamaa simuamini kabisa maacha achelewi kubadilika wawe makini nae

    Jibu

    Mchezo mkali sana huu utakuwa na kwa bernad kulejea uwanjan Ni moja ya changamoto kwa timu pinzan

    Jibu

    Yanga hawajielewi,sijui ni tofauti gani kubwa iliyotokea klabuni na Morrison ila kwa upande wangu Morrison hana nidhamu kabisa.Inawezekana wamemrudisha kambini sababu ya mechi na watani wao wa jadi Simba ila ni upuuzi mtupu.

    Jibu

    Safi arudi awanyooshe tu

    Jibu

    Mamluki huyu wanamkumbatia wa nini

    Jibu

    Duh habar njema kwa mashabik wa yanga upande wa pil usiempenda kaja ngoj tuone JULY 12

    Jibu

    Morrison msumbufu sana anaweza kufanya mazoezi siku ya mechi akajificha kocha asimtegemee sana

    Jibu

    Saf San jembe

    Jibu

    Hana lolote huyo.

    Jibu

    Hyo mechi.itakua bab kubwa Tanzania itasimama siku hyo maana ina hamasa kubwa kwa mashabiki tanzania.kote na ni daby ya vilabu.kutoka jiji moja la Dar es salaam hii si ya kukosa afe kipa afe beki

    Jibu

    Bernard merrison ni mchezaji mzuri Sana ila anamaringo Sana binafsi ningependezwa Kama yanga wakamuza tu

    Jibu

    huyu pasua kichwa sana yaani south Africa hawataki kumsikia ila kakutana na wabongo watu wa miyayusho atakaa sawa

    Jibu

    Hii itakuwa bonge la mechi kwetu sisi mashabiki wa Simba.yanga lazima afungwe siku iyo

    Jibu

    Mmmmm!!!!! Hata haeleweki#Meridianbettz

    Jibu

    Uwenda akaleta mabadiliko

    Jibu

    Kawaida tu

    Jibu

    Habar njema sana 👍

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.