Klabu ya Fenerbahce inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uturuki imesitisha mkataba na mchezaji wake wa kimataifa kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil kabla ya muda wake ambapo mkataba kati yake na klabu hiyo ulikuwa unamalizika mwaka 2024.

Mesut Ozil alijiunga na klabu ya Fenerbahce mwaka 2021 kwa uhamisho huru akitokea klabu ya Arsenal na alisaini kandarasi ya miaka minne, Ozil amefanikiwa kuichezea timu hiyo michezo 37 na kufanikiwa kufunga magoli 9 tu kwa msimu mmoja na nusu aliyoishi kwenye klabu hiyo.

Fenerbahce, Fenerbahce Wam’mwaga Mesut Ozil, Meridianbet

“Tumekubaliana kwamba mkataba kati ya klabu na Mesut Ozil tutauvunja kwa makubaliano ya pande zote mbili. Tunamtakia maisha yenye mafanikio kwenye karia yake.” Waraka wa klabu ya Fenerbahce ulisema.

Kuna taarifa zimekuwa zinasambaa, kuwa nyota huyo wa zamani wa Real Madrid na Arsenal anatarajia kujiunga na klabu ya Istanbul Basaksehir ya nchini Uturuki ambayo nayo inashiriki ligi kuu ya nchini humo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa