Klabu ya Chelsea imethibitisha kumsajiri nyota wa kimataifa wa Uingereza anayekipiga kwenye klabu ya Manchester City Raheem Sterling kwa uhamisho uliogharimu kiasi cha £50million.

Raheem Sterling kwa sasa anajianda kusafiri kwenda nchini marekani kuungana na kikosi cha timu ili kuweza kujufua na timu nzima kwa ajiri ya michezo ya pre-season na kujiandaa na michezo ya ligi kuu ambayo itaanza hivi karibuni.

Raheem Sterling kwa muda wa miaka saba alioutumia kwenye viunga vya Etihad amefanikiwa kucheza michezo 337 na kufunga magoli 131, huku pia akishinda mataji manne ya ligi kuu ya Uingereza.


Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza muda wake wa mapumziko aliutumia nchini Jamaica kabla ya kurudi nchini Uingereza na kufanyiwa vipimo jijini London na sasa yuko nchini Marekani kwenye jimbo la Los Angeles ili kujumuika na timu hiyo.

Raheem Sterling alichapisha barua ya kuaga wote aliofanya nao kazi kwenye klabu ya Manchester City kwenye mitandao ya kijamii.

“Kwa makocha wote ambao walifanya kazi kubwa kwa maendeleo yangu kwa miaka yote hiyo, wachezaji wenzangu ambao tumecheza wote, wafanyakazi na mashabiki ambao waliishabikia timu bila kuchoka, na kila mmoja ambaye anahusika kwenye klabu ya Manchester City, heshima yangu haiwezi kupimika.

“Ni safari ilioje. Nashukuru kwa yote. kwa vipindi vigumu, kuna kipindi, nilijaribiwa uwezo wangu na kushinda, na imeniwezesha mimi kisimama mbele yeni kama toleo bora.

“Niliwasili Manchester nikiwa na umri wa miaka 20, naondoka kama mwanaume. Asanteni kwa mchango usio na kikomo. Ilikuwa heshima kuvaa jersey ya Manchester City.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa