Pape Sakho Akabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Juni

Mchezaji nyota wa klabu ya Simba Pape Sakho leo amekabidhiwa zawadi yake ya mchezaji bora wa mwezi Juni wa klabu hiyo ambapo kiasi cha shilingi milioni mbili amekabidhiwa na kampuni ya Emirate Aluminium.

Pape Sakho ni mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Senegal na alijiunga na klabu ya simba 10 August 2021, tokea Sakho amejiunga na klabu ya simba amekuwa ni moja ya mchezaji muhimu kwenye nafasi ya kiungo wa klabu hiyo.

Pape Sakho alianza maisha yake ya kucheza soka mwaka 2017, kwenye klabu ya Diambars Fc ya Senegal akicheza nusu msimu, Pape msimu wa 2017/2018 alijiunga na klabu ya Mbour P.C kwa uhamisho huru akidumu mwaka mmoja.

Mnamo majira ya kiangazi mwaka 2019, Pape alijiunga na moja ya timu ya daraja la pili nchini Ufaransa na kudumu mwaka mmoja, winga huyu Pape Ousmane Sakho alirejea tena kwenye ligi ya nyumbani na kujiunga na timu ya Teungueth FC na kudumu kwa mwaka mmoja.

Acha ujumbe