FIFA Waruhusu Sabu 5 Katika Mechi

Shirikisho la soka duniani imeamua kutoa kinga ya mda mfupi kwa timu kutumia hadi sabu 5 ili kukumbizana na ratiba ngumu ambazo wanaweza kuwa nazo.

Ligi nyingi zimeathirika na janga la Corona, hivyo inatarajiwa mechi zitakapoanza kuchezwa basi timu zitakuwa na ratiba ngumu za kukimbizana nazo.

Kutokana na changamoto hii, FIFA wamependekeza timu kutumia sabu hadi 5, kwa ligi ambazo zilikuwa zinaruhusu wachezaji pungufu ya hapo. Kinga hii inatarajiwa kuchukuliwa kwa uzito wake na waendeshaji wa ligi na michuano mbalimbali hadi kufikia mwisho wa msimu wa mwaka 2021.

Katika kuzungumzia sababu ya kutoa mapendekezo haya FIFA wanasema hii ni moja ya hatua za kujali afya za wachezaji. Msemaji wa FIFA, anasema kuwa “Afya ndiyo kipaumbele. Hakuna michuano yenye thamani ya kuhatarisha maisha hata ya mtu mmoja.”

Shirikisho hili limesisitiza kuwa michuano ya soka inapaswa kuendelea pale tu taasisi za afya na mamlaka za serikali zitakapotoa taarifa kuwa mazingira yaliyopo ni rafiki kwa michuano kuendelea kwa kuzingatia afya za wachezaji na wadau wengine.

Kutokana na hofu kuwa mechi nyingi zilizopo zitaoperekea ratiba inayohitaji kasi, pia kuna uwezekano wa kuongezeka kwa majeraha ya wachezaji, mapendekezo haya ni namna ya kupunguza hatari inayoweza kutokea.

Hata hivyo, mapendekezo haya yanahitaji kupitiwa na kupitishwa na bodi ya SHirikisho la Soka la kimataifa (IFAB).

4 Komentara

    FIFA watuachie uhondo wa mechi urudi

    Jibu

    Nijambo zuri FIFA waliloamua kuweka sababu ili pasitokee malalamiko

    Jibu

    habar njema

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe