Victor Wanyama: Amrouche Alipwe Haraka Iwezekanavyo

Nahodha wa Harambee Stars Victor Wanyama amelitaka Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kumaliza deni la kocha Adel Amrouche haraka iwezekanavyo. Shirikisho hilo linadaiwa na kocha wake wa zamani raia wa Algeria baada ya kumfukuza bila kufata Sheria na baada ya kocha huyo kwenda kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo, iliamuliwa FKF kumlipa kocha huyo $1M (Bilioni 2.3 Tsh), FIFA imeongeza muda zaidi kwa FKF hadi kufikia mwezi Mei kuwa imelipa pesa hizo.

Victor Wanyama

Akiongea na BBC, Wanyama amesema kuwa kama Kenya itafungiwa kutoshiriki michezo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia haitakuwa hathari kwa soka la Kenya tu lakini hata kwa wachezaji ambao wangetaka kuonyesha uwezo wao katika soka la ulimwengu. “Ni aibu kuwa kitu kama hicho kinaweza kugharimu wachezaji wengi fursa ya kushiriki kwenye michuano mikubwa ulimwenguni. Nataka kuwasihi FKF tafadhali tafuta njia ya kushughulikia suala hilo haraka ili tuweze kuendelea na ndoto yetu ya kuwa kwenye michuano mikubwa ulimwenguni, “Wanyama amesema.

Katika safari yao ya kufuzu Kombe la Dunia 2022, Kenya imepangwa katika kundi moja na Mali, majirani Uganda na Rwanda na kulingana na Wanyama wasingeweza kupoteza nafasi kama hii ya kuandika historia ya kufuzu kombe la Dunia kwa mara ya kwanza. “Nadhani tunayo nafasi ya kufuzu. Lakini ukweli ni kuwa tunaweza kupigwa marufuku na FIFA kwa sababu ya pesa anadai kocha wetu wa zamani,”

Wanyama ambaye aliongoza timu hiyo kwenye fainali za AFCON 2019 hivi sasa anacheza soka katika Ligi ya Marekani MLS kwenye klabu ya Montreal Impact baada ya kutoka Spurs mapema mwaka huu

4 Komentara

    That’s is a true Legendary!!!!!

    Jibu

    Wamlipe haraka ili East Africa tuwe na muwakilishi

    Jibu

    Apewe haki yake

    Jibu

    Wamlipe tu .

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.