Klabu ya Borussia Dortmund wametanga Edin Terzic kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo ambapo atahudumu kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2025 kufuatiwa kuondoka kwa kocha wao Marco Rose.
Edin Terzic aliwai kuwa kocha wa muda wa klabu hiyo kuanzia December 2020 hadi May 2021 na alifanikiwa kuiongoza Borussia Dortmund kushinda kombe la Ujerumani.
Terzic ambaye alikuwa msaidizi wa Lucien Favre mwaka 2018. Lucien Favre alipofungashiwa virago alichukua nafasi yake ya kama kocha wa muda hadi msimu kuisha na kupatiwa kazi ya mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Borussia Dortmund
Baada ya kutangaza alisema, “kwa sasa watu wanapaswa kujua ni kwa kiasi gani BVB ni muhumi kwenye maisha yangu, tutatoa kila kitu kila siku kwa ajiri ya mafanikio ya klabu hii.”
Pia mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Sebastian Kehl alisema, “tumeshawishika kwamba maamuzi haya sisi kama timu ni maamuzi sahihi kwa Dortmund, Edin anaijua hii klabu, mazingira na sehemu kubwa ya timu na marekebisho ambayo tunata kufanya ili kuweza kufanikiwa kwa ajiri ya mashabiki wetu.”
Edin Terzic alishawai kuwa kocha msaidizi wa Dortmund U19 2010/11, Skauti wa klabu, 2010/2013, kocha msaidizi wa timu B 2011, kocha mkuu wa wa chini ya 16 2013, kocha msaidi wa chini ya 17 2011/13, kocha msidizi wa Besiktas 2013/15, kocha msaidizi wa West Ham 2015/17 baada ya hapo akarudi tena BVB tena.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.