De Ligt: Sina Mpango wa Kuondoka Bayern

Beki wa kimataifa wa Uholanzi Matthijs De Ligt ameweka wazi hana mpango wa kuondoka ndani ya viunga vya Allianz Arena na badala yake ataendelea kuitumikia klabu hiyo.

De Ligt amekanusha tetesi za kua ana mpango wa kuondoka ndani ya klabu ya Bayern Munich na kusisitiza kua bado yupo ndani ya klabu hiyo kwakua ana furaha kuendelea kuwatumikia Bavarians.de ligtBeki huyo wa zamani wa vilabu vya Ajax na Juventus amekua anapitia kwenye kipindi kigumu ndani ya klabu hiyo kwa kukosa nafasi ndani ya kikosi hicho, Licha ya kukosa nafasi ya kuanza mara kwa mara klabuni hapo lakini bado beki huyo hafikirii kuondoka klabuni hapo.

Beki De Ligt amesema klabu hiyo na mashabiki kwa ujumla wamekua wakimuonesha upendo mkubwa, Hivo anafurahi kua mahala hapo kutokana na upendo na ushirkiano ambao amekua akiupata kwa klabu na mashabiki wa klabu hiyo.de ligtBeki anaonekana kua na matumaini ya kurejesha nafai ndani ya kikosi hicho kwani kocha aliyepo kwasasa Thomas Tuchel ambaye amekua hampi nafasi mara kwa mara ataondoka mwishoni mwa msimu huu, Hivo hii inaweza kua imempa matumaini beki huyo kuamini anaweza kupata nafasi ya kucheza kwa kocha ajaye.

Acha ujumbe