Bingwa wa ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 wanampango wa kumfuta kazi kocha wa klabu hiyo Mauricio Pochettino siku kadhaa baada ya kufanikiwa kuipa ubingwa msimu huu ikiwa sehemu ya kufanya maboresho ya klabu hiyo.

Mauricio Pochettino amekuwa kwenye klabu ya PSG kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, mkataba wake unatarajiwa kumaliza mwishoni mwa msimu ujao, lakini PSG wanatarajia kusitisha mkataba wake mapema zaidi.

PSG

Habari za klabu ya kusitisha mkataba zimetoka mapema baada ya PSG kuchukua ubingwa wao wa kumi  na ubingwa wa kwanza kwa Mauricio Pochettino tokea achukue hatamu ya kuinoa klabu hiyo, licha ya kuwa na msimu mgumu.

Ukiondoa kocha huyo pia klabu ya PSG inampango wa kumfuta kazi mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Leonardo, ambaye mafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na  mkurugenzi wa zamani wa klabu za Monaco na Lille Luis Campos.

Luis Campos ni moja ya rafiki mkubwa wa familia ya Mbappe ambae alikuwa na kazi kuendeleza kipaji cha mshindi huyo wa kombe la dunia kipindi akiwa nae kwenye klabu ya Monaco.

Nafasi ya Mauricio Pochettino kwenye klabu ya PSG kuna tetesi ya kuwa Zinedine Zidane ndiye ambaye anatakiwa kurithi mikoba hiyo, japokuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliofanyika na kocha mpaka sasa.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa