Historia inaonesha kuwa Michezo ya Olimpiki ilianza zaidi ya miaka 3,000 iliyopita katika mji wa Olympia, Kusini Magharibi mwa nchi ya Ugiriki.
Madhumuni ya michezo hii ilikuwa ni tamasha la kidini, kumtukuza Zeus ambaye alikuwa ni Mfalme wa miungu nchini humo na ilikuwa inafanyika kila baada ya miaka minne.
Wakati huo, watu wote nchini Ugiriki walishiriki kwa pamoja katika tamasha hilo mbele ya Mfalme huyo.
Lakini mwaka 1896, michezo ya kisasa ya Olimpiki yalifanyika kwa mara ya kwanza jijini Athens.
Mwaka huo, wanamichezo 280 wote wakiwa wanaume kutoka mataifa 13 walishiriki katika michezo 43.
Michezo ambayo ilishindaniwa wakati huo ni pamoja na kukimbiza baiskeli, Tennis na unyanyuaji wa vyuma miongoni mwa michezo nyingine.
Vita vya dunia vilisababisha michezo hiyo kutofanyika mwaka 1916, 1940 na 1944, huku nchi nyingi zikijiondoa kushiriki katika michezo ya mwaka 1980 na 1984 kwa sababu ya vita baridi vya dunia.
Hata hivyo, ilipofika mwaka 1994 michezo hii iligawanywa mara mbili ile ya msimu wa joto na baridi, na tofauti ya michezo hiyo ilikuwa ni miaka 2.
Michezo hii inasimamiwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ambayo ina jukumu la kuandaa michezo hii, ikiwa ni pamoja na kutafuta mji wa kuandaa michezo hiyo lakini pia kutafuta fedha za kuifadhili.

Ishara ya michezo hii ni bendera na mwenge.
Michezo hii pia hutoa nafasi kwa nchi na mji unaoandaa michezo ya Olimpiki kujitangaza kwa dunia na kuonesha mambo yake kwa maelfu ya wageni wanaohudhuria michezo hii.
Ni michezo ambayo pia katika historia yake imekuwa ikitawaliwa na ususiaji, wanamichezo kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini ili kushinda, ufisadi na hata shambulizi la kigaidi.
Mwaka 1972 wakati michezo hii ilipofanyika mjini Munich nchini Ujerumani, wakati huo ikiwa ni Ujerumani Magharibi, wanamichezo na maafisa wa Israel 11 walitekwa na kuuawa na kundi la kigaidi kutoka Palestina.

Mshindi wa kwanza katika michezo mbalimbali hutuzwa medali ya dhahabu, mshindi wa pili medali ya fedha na mshindi wa tatu medali ya shaba.
Wanamichezo walemavu pia wamepata nafasi ya kushiriki katika michezo hii tangu mwaka 1960, lengo lilikuwa ni kuwapa nafasi wanajeshi waliokuwa wamejeruhiwa na kuwa walemavu baada ya vita vya dunia kuonesha vipaji vyao katika michezo mbalimbali.

Michezo ya walemavu hufanyika kipindi cha joto kila mwaka wakati wa michezo ya kawaida ya Olimpiki ya majira hayo.
Bara la Afrika halijawahi kupata fursa ya kuwa mwenyeji wa michezo hii.
Marekani ndio nchi peke duniani ambayo imeandaa michezo hii mara nyingi ikiwa ni mara 8.
Kipindi cha joto Marekani imekuwa mwenyeji mwaka 1904,1932,1984 na 1996 huku yale ya kipindi cha baridi yakifanyika mara nne pia mwaka 1932,1960,1980 na 2002.
Miji ambayo imekuwa maarufu kuandaa michezo hii ni Los Angeles na Lake Placid.
Ufaransa nayo imeandaa mara 5, Japan mara 4 huku Uingereza, Canada , Italia na Ujerumani ikiandaa mara 3.


Isaya massawe
Taarifa nzuri sana hizi sikujua mapema kabla
Johnmary joel
Nilikuwa sijui historia ya mchezo huu#meridianbett
Amani
Hii nouma Sana kwa Mara ya kwanza
Nilikuwa sijui historia ya mchezo huu#meridianbett
Neema juma
Kumbe ndoilivyoanza anza hii ni historia nzuri
isha
Duuh hii hatari sana kumbe hii ndio history ya mchezo huu
Sadick
Ni michezo ya yenye historia ndefu ya kuvutia#meridianbettz
JULIANA
Asante kwakunijuza mengineyo nisiyo yajua
Khadija
duuh kumbe hii ndio historia ya huu mchezo#meridianbettz
Povel
Habar njema
Genia Sikaluzwe
Ahsant kwa habari
Zeiyana
Asante kwa kutujuza
Dorophina
Nilikuwa sijajua hii tnx meridian kwa kutujuza
Franky
Safi sana ni taharifa nzuri pia kuusiana na mashindano haya…
Rehema Dickson
Habari nzuri asante meridian kwa kunijua sikua nalijia hili kabla
felister
ahsante kwa taarifa
Lydia Emmanuel Magoti
Tarifa nzuri Sana kwasisi wateja kutujuza
Caroline
Kumbe ni muda mrefu eeh
Magdalena
Habari mashughuli izi
Ester jackson
Good news
Edgar
Safi sana meridian kwa makala nzuri na kujua baadhi ya Mambo kuhusiana na uanzilishi wa michezo ya onlimpic..
Ernest
Nafurahi kuwa mteja wa Meridianbet kwani nakuwa mjanja kwa updates na historia mbalimbali
Mwanahamisi
Asante kwa taarifa
warda
Ipo Siku Africa Tutakuwa Wenyeji wa mchezo huu#Meridianbettz
nasra
Sikuwa nafahamu asantee kwa taarifa meridianbet
Fatina mfingi
Asanteh kwa taarifa
Hamidu
Asante kwa update za michezo#meridianbettz
Samiah
Asanteee kwa taarifa
Njiku
Michezo mizuri sanaa
Hope mwaikuka
Axante maana nlkua cjui kuhusu ili
Gabriel
Historia nzur sana hii nimeipenda
Issa
Olimpiki ni michezo inaaokutanisha wanamichezo pamoja
Angelina
Makala nzuri sana
fatumakasom
Nimichezo yenye kihistoria ndefu
Furahav
Habari nzuri.
Saupha mohamed
Good news
Rehema
Nilikuwa sifaham meridianbet asante
Amiri Kayera
Thanx meridianbettz Kwa kutujuza
Devotha
Asanteni kwa kutujuza historia ya mchezo huu
Latifa juma mohamed
Ni michezo ya kuvutia Sana
Salma
Hii safi sana
Theckla
Meridianbette mko vizuri mm sikuwa najua vizuri hili
Omary lukumbi
Duu asanten meridian maana nilikua sijui mashindano ya Olympic yalipo anzia na kwa mwaka gan
Evaluziga
Ni habari njema
David Pere
Wagiriki kweli noma waliza nini kuanzisha haya mashindano
Theonestina
Habar mzur Sana jamani
Mariam mtandama
Habari njema
Shafii
Gud newz
Sabrina
Maoni:Nashukuru kwa kunifahamisha historia ya michezo ya olimpiki.
mwakalosi
Ugiriki ina history pana sana
lombo
saf