LICHA ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano ‘Playoff’ dhidi ya JKT Tanzania benchi la ufundi la Tanzania Prisons limehofia mchezo wa marudiano.

Mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kupigwa Julai 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, huku Prisons wakiwa na faida ya bao moja lililofungwa kwenye Uwanja wa Isamuhyo jijini Dar es salaam.

Tanzania Prisons, Tanzania Prisons Yaihofia JKT Tanzania, Meridianbet

Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Patrick Odhiambo alisema “Wachezaji wapo katika hali nzuri na tunaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo unaofuata.

“Huu mchezo unaofuata ndio utakuwa mgumu zaidi kwetu kushinda, ule wa kwanza tulifanikiwa kupata matokeo, ila mchezo huu JKT watakuja na mbinu nyingine kwani hawana kitu cha kupoteza.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa