Real Wanaendelea Kuwa Wateja!

Real Madrid wameshindwa kulipa kisasi, badala yake wanaendelea kuwa wateja tu kwa Barcelona baada kukubali tena kichapo cha bao 1-0 kwenye dimba lao kutoka kwa Barcelona! El clasico iliyopita Real Madrid walichapwa bao 3 bila.

Barcelona wamefanikiwa kufikia tofauti ya pointi 10 kileleni kwenye LaLiga baada ya kushinda El Clasico ya pili siku 4 tuu baada ya ile ya kwanza kwa mwaka huu. Ivan Rakitik amefifisha matumaini ya kutwaa taji ya Real Madrid kwa sasa. Barcelona wameshinda El Clasico 4 mfululizo na kuvunja rekodi ya kuongoza kushinda dhidi ya Real Madrid.

Real Wanaendelea Kuwa Wateja!
Barcaleona wameshinda jumla ya gemu 96 na Real wameshinda 95. Barca wanaongoza kwa mara ya kwanza kutoka mwaka 1932

Real Madrid wamebakia nafasi ya tatu wakiwa nyuma kwa pointi 12 zaidi kwa Barcelona ambao ndio vinara huku wakiwa na gemu 12 mkononi. Atletico Madric wanatarajia kupunguza gepu la pointi 3 kama watafanikiwa kushinda gemu dhidi ya Real Sociedad leo.

Real walijitahidi kuonyesha soka bora zaidi baada ya kushindwa kuinasa Copa de Rey, kama wangefanikiwa kushinda gemu hii wangejiongezea matumaini ya kupambania taji kwenye Ligi. Solari anasisitiza kuwa kwa sasa ligi hiyo kwao bado ni muhimu na klabu hiyo itajitahidi kupambana hadi dakika ya mwisho.

2 Komentara

    Mpira hauna mwenyewe.

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe