Kocha wa klabu ya Fc Barcelona Xavi Hernandez amewatoa hofu wachezaji wake na kuwataka kujua kua mchezo wao wa jumapili dhidi ya Atletico Madrid hautaamua chochote kuhusu ubingwa msimu huu.

Kocha Xavi ameongea hayo ili kushusha presha za wachezaji kuelekea mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid ambapo watakua ugenini na kutaka wachezaji wake waelewe matokeo yoyote yatakayopatikana katika mchezo huo hayatatoa taswira ya ubingwa.XaviKlabu ya Fc Barcelona ambayo wao wametoka sare katika mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu nchini Hispania dhidi ya mahasimu wao Espanyol, Na kuwafanya kudondosha alama mbili ambazo zilifanya wapinzani wao klabu ya Real Madrid kuwafikia kwa alama.

Lakini kocha Xavi ameweka wazi kua kupoteza alama katika mchezo dhidi ya Atletico Madrid itakua pigo kubwa, Ni wazi kocha huyo anataka kuondoa presha kwa wachezaji wake kuelekea mchezo huo lakini pia anajua wakipoteza alama katika mchezo huo itakua ni pigo zaidi kwa upande wao.XaviKlabu ya Real Madrid wao wanakipiga leo dhidi ya klabu ya Villarreal ugenini katika dimba la Estadio de le Ceramica, Hivo klabu hiyo ikishinda itakaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo huku klabu ya Barcelona wakipoteza mchezo wao wa kesho basi watabaki katika nafasi ya pili.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa