Klabu ya Real Madrid leo itashuka dimbani katika mchezo wa 16 wa ligi kuu ya soka nchini Hispania La liga dhidi ya klabu ya Villarreal katika dimba la Estadio de le Ceramica.

Klabu ya Real Madrid leo watakua ugenini dhidi ya klabu ya Villarreal ambapo watakua wakitafuta nafasi ya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo dhidi ya klabu ya Barcelona ambao ndio wanaongoza ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.Real MadridVijana wa Carlo Ancelotti watahitaji alama tatu muhimu ambazo zitawafanya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ili kuendeleza kampeni ya kutetea ubingwa huo ambao mpaka sasa klabu hiyo ndio mabingwa watetezi  wa kombe la La liga nchini Hispania.

Klabu ya Real Madrid haijafanikiwa kushinda ugenini dhidi ya Villarreal na mara ya mwisho ilikua mwaka 2017 ikiwa imepita takribani miaka sita sasa, Hivo wanajua kua wazi kua mchezo wa leo ni mgumu kwelikweli kwa upande wao.Real MadridKlabu ya Villarreal wao ambao wanaanza maisha mapya bila ya kocha wao Unai Emery alietimkia klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza, wao wana kazi moja tu ya kulinda rekodi yao ya kutokufungwa na Madrid katka dimba lao la nyumbani toka mwaka 2017.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa