Mtoto wa mfalme wa Saudia Arabia Mohammed Bin Salman Al Saud ametangaza kila mchezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo kuzawadiwa gari la aina ya Rolls Royce. Hiyo ni baada ya kushinda mchezo wao wa kombe la dunia siku ya jumanne dhidi ya Argrntina.
Timu ya taifa ya Saudia Arabia ilishtusha dunia baada ya kuifunga timu ya taifa ya Argentina siku ya jumanne kwa mabao mawili kwa moja. Watu wengi walishangazwa kutoka na timu hiyo kutopewa na nafasi na kuifunga timu ambayo inapewa nafasi ya kubeba ubingwa kutokana na ubora iliokua nao.Mtoto wa mfalme wa nchi hiyo ametoa zawadi hiyo ambayo itagharimu kiasi cha bilioni 3 kwa kila gari, Ikumbukwe Rolls Royce ni miongoni mwa magari ya kifahari na yenye thamani zaidi duniani.
Saudia Arabia kama nchi wamepokea ushindi huu kwa uzito mkubwa kwani baada ya ushindi huo mfalme wa nchi hiyo alitangaza mapumziko siku inayofuata kwa taifa zima na kuonesha ni namna gani kama nchi wamfurahishwa na ushindi huo.Timu hiyo ambayo ipo chini ya kocha wa zamani wa Zambia Herve Renard inatarajiwa kucheza mchezo wa pili wa michuano hiyo dhidi ya timu ya taifa ya Poland, Na kama watafanikiwa kupata matokeo ya ushindi basi watakua wamejihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.