Timu ya Taifa ya Uholanzi leo itajitupa uwanjani kukabiliana na timu ya taifa ya Ecuador katika mchezo wa pili wa kundi A. Kama timu hiyo itashinda mchezo wa leo basi itakua imejihakikishia kufuzu hatua ya 16.
Timu hizo zinakutana huku zikiwa zimelingana kwenye kila kitu kwani Ecuador wana alama tatu na magoli mawili huku Uholanzi nao wakiwa wameshinda mchezo wa kwanza kwa magoli mawili kwa bila dhidi ya Senegal.Vijana wa Louis Van Gaal wameonesha hali ya upambanaji katika mchezo wa kwanza dhidi ya Senegal kitu ambacho kinaweza kuwapa morali ya kupata ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya timu ya taifa ya Ecuador.
Ecuador ambao nao wameonekana kua na kiwango bora sana katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya wenyeji Qatar, Hivo inaonekana ni wapinzani ambao wanaweza kuleta ushindani mkubwa katika mchezo huo.Uholanzi walikosa michuano ya kombe la dunia 2018 pale Urusi na kurudi kwao kwenye michuano hiyo mwaka huu inakua kivutio kwani wamekua timu yenye ushindani kila wanaposhiriki michuano ya kombe la dunia.