Kichapo cha 1-0 kutoka Atletico Madrid kiliiondoa timu Man United kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, na kuwafanya wawe na msimu wa tano mfululizo bila ya kupata taji, huku Ronaldo akiwa hana taji kwa miaka 17.
Wakati United wakipoteza, ilikuwa ni siku mbaya kwa Ronaldo kwani hakuwa na shuti hata moja kwenye mechi hiyo, ikiwa ni mara ya tatu tu kushindwa kufanya hivyo kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa na ikiwa ni mara ya kwanza tangu 2011 alipoichezea Real Madrid dhidi ya Barcelona.
Kipindi cha pili cha Ronaldo huko Old Trafford kinaanza kuonekana kama jinamizi baya. Lakini usajili wa makinda kama Haaland na Kylian Mbappe unaweza kuleta matumaini klabuni hapo?
Huku kukiwa hakuna taji lolote linalokuja Old Trafford msimu huu, klabu hiyo sasa ina lengo moja – kuhakikisha inarejea Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Hata hivyo, hata hilo halipo mikononi mwao kwani kwa sasa wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, pointi moja nyuma ya Arsenal, ambao wana mechi tatu mkononi.
Huku hali ya kiwango cha klabu ikiwa chini sana, kuna mengi ya kufanywa ili kuwarejesha mabingwa hao mara 20 wa ligi pale walipokuwa.
Malejendari wa klabu Rio Ferdinand na Paul Scholes wanadhani kusajili makinda kama Erling Haaland au Kylian Mbappe haingetosha kuifanya Man United kuwa timu iliyoshinda tena taji.
Rio Ferdinand says that even Mbappe and Haaland won’t solve the problems that start at the top for Manchester United 😮 pic.twitter.com/66qIwFbUPh
— ESPN FC (@ESPNFC) March 15, 2022
SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.


