Nahodha wa zamani wa Liverpool na kiungo mkongwe wa England, Jordan Henderson, ameachana rasmi na klabu ya Ajax baada ya kuamua kutoongeza mkataba wake wa mwaka mmoja zaidi, ambao ungeendelea hadi mwaka 2026.

Henderson, mwenye umri wa miaka 34, alijiunga na Ajax mwezi Januari 2024 kwa mkataba wa miezi 18 baada ya kipindi kifupi kisicho na mafanikio sana katika Ligi ya Saudi Arabia. Akiwa Ajax, alicheza mechi 37 na kufunga bao moja, huku akipewa pia unahodha na kocha mpya Francesco Farioli – jambo lililodhihirisha umuhimu wake ndani ya kikosi.
Licha ya Ajax kuwa na haki ya kumwongezea mkataba, yeye mwenyewe ameamua kuondoka kwa hiari na sasa ni mchezaji huru, hali inayomuweka sokoni kwa vilabu vinavyohitaji uzoefu mkubwa katikati ya uwanja.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Nini Kinafuata kwa Henderson?
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Uingereza, vilabu kadhaa vya Premier League tayari vinaonyesha nia ya kumsajili kiungo huyo. Henderson anadaiwa kuwa na nia ya kurudi Uingereza ili aweze kuongeza nafasi zake kwenye kikosi cha England kuelekea Kombe la Dunia la 2026.

Henderson anatafuta timu ambayo itampa nafasi ya kucheza mara kwa mara na kuchangia mafanikio ya klabu huku akiweka jicho kwenye michuano ya kimataifa kwa mara nyingine.

