Juventus wanatajwa kuwa wameainisha meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane kama kipaumbele katika kumsaka nani anaweza kuwa mrithi wa Andrea Pirlo Juventus.
Pirlo amekuwa na kipindi kigumu msimu huu, ikiwa ni mwaka wake wa kwanza kama meneja Juventus wakati Juventus wakishindwa kutoboa Ligi ya Mabingwa na kuwa nyuma kwenye mbio za kuwania taji msimu huu.
Kwa mujibu wa Daily Mail, meneja Zidane alikuwa chaguo la kwanza la Juventus wakati Massimo Allegri alipoonka Juventus miaka miwili iliyopita, na hilo halijabadilika.
Baada ya kushindwa kumuondoa Zidane kutoka Madrid, basi Maurizio Sarri akauchukuliwa kama mbadala, naye baada ya kuondoka basi Pirlo akachukua kijiti, lakini wote wanaonekana kuwa wanaishia kwenye kushika majukumu kwa semister moja tu.

Mwenyekiti wa Juventus, bado ana imani kuwa Zinedine ndiye mbadala sahihi wa Pirlo pale Juventus. Licha ya kuwa na mafanikio makubwa pale Madrid, Zidane hajawa akipata sapoti ya kutosha hasa kipindi hiki cha hivi karibuni.
Klabu inaamini kuwa wanalo kundi kubwa la wachezaji ambao wanaweza kupambana vyema kwenye Ligi ya Mabingwa na kutawala soka la Italia, lakini wanahitaji mtu ambaye ataweza kuwatumia vyeama zaidi, hivyo mfaransa huyo anaonekana kuwa katika nafasi nzuri kwenye hili.
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



dorophina
Itakuwa poa sana
Sarah
Safi sana
Venerose
Inapendeza
Angelina
Iko vizuri
Hopemwaikuka
Sawaa
warda
Mi huwa namkubali sana Zidane