Lionel Messi Anatamani Kucheza Marekani

Baada ya harakati za kutaka kuondoka Barcelona kutozaa matunda. Lionel Messi atamka hadharani matamanio yake ya kucheza Ligi Soka nchini Marekani – MLS.

Lionel Messi aliutikisa ulimwengu wa soka baada ya kuwasilisha ombi la kuondoka Barcelona mwezi Augosti. Licha ya kwamba ombi lake halikufanikiwa, Messi anaendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu mkataba wake utakapoisha.

Messi amekuwa akihusishwa na vilabu mbalimbali kama vile Man City na PSG lakini kugusia suala la kucheza Marekani, pengine litaibua picha nyingine.

Lionel Messi
Lionel Messi

Akizungumza na kituo cha televisheni cha La Sexta nchini Hispania, Lionel Messi amesema “bado sijajua nitafanya nini.

“Nitasubiri mpaka mwishoni mwa msimu. Ningependa kwenda kucheza Marekani na kujifunza maisha na ligi ya kule lakini nitarudi Barcelona kwa kiasi fulani.

“Kwa sasa ninaiangalia zaidi Barcelona na kumaliza msimu huu vizuri, lengo ni kushinda mataji na sio kuyumbishwa na mambo mengine.”

Msimu uliopita, Barcelona hawakubeba taji lolote na wanashikilia nafasi ya 5 kwenye msimamo wa La Liga msimu huu. Huu ni mwanzo mbaya kwa miamba ya Catalunya na ni historia baada ya miaka 33.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

13 Komentara

    Wako juu

    Jibu

    Kipajai anacho ana haki ya kuchezea timu yeyote ile duniani

    Jibu

    Yuko vizuri lazima atambe

    Jibu

    Itakuwa vizuri mess akiahama Barcelona

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

    Messi akitaka kwenda kokote hakuna sehemu watamkataa kutokana na uwezo wake

    Jibu

    Yuko poa

    Jibu

    Sio mbaya kubadlisha mazingra

    Jibu

    Messi Yuko vizuri na anakubalika

    Jibu

    Messi atulie tu barcelona

    Jibu

    Messi anaweza kuongea kitu chochote kwasababu yeye nimchezaji anae jiamini

    Jibu

    Saf kwake

    Jibu

    Atacheza tu ni swala la mda

    Jibu

Acha ujumbe