Lucas Vazquez amesaini mkataba wa miaka mitatu na Real Madrid na mhispania huyo amesema kwamba atakuwa na nafasi ya kuongeza historia ndani ya klabu hiyo.
Baada ya kumwaga wino kwenye mkataba mpya alijadili mafanikio na kila kitu anachotarajia kukipata ndani miaka ijayo akiwa na Los Blancos.
“Hii inamaana kubwa kwangu na ninajivunia, ni maalumu,” alisema baada ya kusaini makataba mpya Media Real Madrid.
“Ndoto yangu inaendelea hapa, ambayo ni nyumba yangu, na kitu ambacho nahisi ni sehemu yangu sana. Wewe huwa unaota mambo makubwa, lakini ni ngumu kuendelea na kuyafanikisha.
“Nimefurahi sana kuongeza mkataba wangu na kufurahiya kuwa mchezaji wa Real Madrid hadi 2024. Mimi ni mchezaji wa klabu ambaye nimekua na maadili ya Real Madrid na hii inafanya familia yangu na mimi kufurahi sana.
“Real Madrid wana maadili yaliyowekwa vizuri: kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu wengine, unyenyekevu … Haya mambo hayawezi kujadiliwa maishani na kwenye mpira.
“Nimecheza mara 240 lakini nitapambana kuhakikisha kuwa kuna mengi zaidi yajayo.”
MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Good
Vizuri