Mchezo wa magwiji wa klabu ya Manchester United dhidi ya Liverpool uliopigwa katika dimba la Anfield jana uliisha kwa magwiji wa klabu ya United kufungwa mabao mawili kwa moja.

Licha ya magwiji wa Man United kutangulia kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa Bulgaria Dimitar Bebertov ila haikua sababu ya kuepuka kipigo dhidi ya magwiji wa hao wa Anfield.

magwijiMagwiji wa Liverpool walirudi mchezoni kipindi cha pili baada ya kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao moja ndipo mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Mark Gonzalez kufanya ubao kusomeka bao moja kwa moja kabla ya Sinama Pongolle kuongeza bao la pili na kufanya mchezo huo wa magwiji wa kaskazini kuishi kwa goli mbili kwa moja.

magwijiMchezo huo ambao ulifanya wapenzi wa soka kuona wachezaji wao vipenzi wa zamani kama Xabi Alonso ambae anareje klabuni hapo baada ya muda mrefu kupita akiwa kama nahodha kwenye mchezo huo,Halikadhalika mchezaji wa zamani wa Man United kiungo mtukutu Roy Keane ambaye aliingia kipindi cha pili cha mchezo huo.

Tukio lililoibua mijadala katika mchezo huo ni pale gwiji Roy Keane alipoingia kipindi cha pili na mashabiki wa Liverpool kuanza kumzomea ikionesha bado wanakumbuka fujo za gwiji huyo na maneno yake makali dhidi ya mahasimu wake hao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa