Klabu ya Manchester City imekamilisha uhamisho wa kiungo wa Yui Hasegawa kutoka West Ham kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Kiuongo huyo wa kimataifa kutoka Japan amefanikiwa kufunga mara mbili tu kwenye michezo 17 aliyoichezea klabu ya West Ham tangu ajiunge nayo August 2021 akitokea AC Milan.

Manchester City, Manchester City Yamsajiri Kiungo wa Kijapan, Meridianbet

“Nilipocheza dhidi ya Manchester City msimu uliopita, kiukweli nilipenda jinsi timu ilivyokuwa ikicheza, Hivyo nilivyopata nafasi, Haraka nilitaka kujiunga na klabu. Aalisema.

“Watu wananiona kama mshambuliaji lakini pia nataka nitambulike kama mlinzi na kutotabirika. Naweza kuwa mdogo lakini niko imara na nataka kuwaonesha hilo.

“Ningependa kutengeneza magoli na kusaidia kupataikana magoli mengi kwa timu kadri iwezekanavyo msimu huu, natumai tutafurahia mafanikio mengi.”

Kocha wa wanawake wa klabu ya Manchester City Gareth Taylor alisema kuwa alikuwa anamuhusudu kwa muda mrefu “kiungo mshambuliaji aliyebarikiwa”.

“Tunajiandaa kufanya kazi Yui kwa msimu huu na kuona jinsi atakavyo acha alama kwenye Jersey ya Manchester City.”

aliongozea

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa