Klabu ya Manchester City itaendelea kuwakosa nyota wake watatu wa kikosi cha kwanza kuelekea mchezo wao wa ligi kuu ya Uingereza utakaopigwa kesho dhidi ya klabu ya Aston Villa.
Wachezaji kama beki Nathan Ake, golikipa Ederson Moraes, pamoja na beki wa kulia Kylie Walker ni wachezaji ambao watakosekana katika mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Uingereza ambao utakwenda kupigwa katika dimba la Etihad.Beki Nathan Ake alikuepo katika mchezo wa wikiendi iliyomalizika dhidi ya Arsenal lakini alishindwa kumaliza mchezo kutokana na majeraha ambayo aliyapata katika mchezo huo na kumfanya kuungana na majeruhi wengine kama Walker na Ederson.
Wachezaji hao ambao wamekua mhimili wa klabu ya Manchester City kukosekana kwao katika mchezo huo dhidi ya Villa ni pigo kwa klabu hiyo, Kwani wamekua na mchango mkubwa sana katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo.Baada ya taarifa hiyo kutoka ambayo sio nzuri kwa mashabiki wa klabu ya Manchester City, Lakini taarifa njema ni kua beki mwingine wa klabu hiyo ambaye muda mwingine anatumika kama kiungo John Stones amerejea kutoka kwenye majeraha na anaweza kua sehemu ya kikosi kesho.