Mchezo wa kibabe kabisa ambao ulikua unasubiriwa na mashabiki wa soka kati ya klabu ya Manchester City dhidi ya Arsenal umemalizika kwa sare ya bila kufungana jioni hii.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Etihad ulishuhudia miamba hiyo ya soka kutoka nchini Uingereza ikitoshana nguvu wakigombania nafasi ya kua juu ya msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.Manchester City walionekana kutawala mchezo kwa kiwango kikubwa huku klabu ya Arsenal wao mara nyingi wakiwa wanazuia kwa nidhamu ya hali ya juu kuhakikisha vijana wa kocha Pep Guardiola hawaeki mpira wavuni kwenye goli lao.
Vilabu vyote viwili vipo kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza mpaka wakati huu na ni wazi timu zote zilikua zinahitaji matokeo katika mchezo wa leo, Lakini mchezo umemalizika na sare na hakuna aliefanikiwa kupata alama tatu.Baada ya sare ya bila kufungana kati ya Manchester City na klabu ya Arsenal imetoa fursa kwa klabu ya Liverpool kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Kwani wao wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Brighton leo.