Manchester City Wamebamizwa Tena
Makala iliyopita
Manchester United ya Asali na Maziwa imerejea
Liverpool wakiwa nyumbani walionekana wanahitaji kuendeleza kile ambacho wamekua wakikifanya msimu huu kwa ubora mkubwa, Kwani walianza kwa kasi wakiliandama lango la Man City na mapema dakika ya 12 tu Coady Gapko aliipatia bao la kuongoza Liverpool akipokea pasi nzuri ya Mohamed Salah na kuwapa uongozi majogoo wa Anfield.
Kipindi cha pili Liverpool walionekana kuendelea kutawala mchezo na kutengeneza nafasi za mabao huku ugonjwa wa kipindi cha kwanza ukiendelea kushindwa kuzitumia nafasi mpaka pale dakika ya 77 Luis Diaz kuchezewa madhambi kwenye eneo la hatari na Mohamed kufunga bao dakika ya 78 ya mchezo na kufanya ubao kusomeka mabao mawili kwa bila.