Baada ya kupambana kuitafuta tiketi ya kushiriki Michuano ya Ulaya – UEFA msimu ujao. Sasa Manchester United wanaelekea kwenye michezo ya mwisho kunako kombe la Europa.
Manchester United walimaliza msimu wa Ligi Kuu Uingereza – EPL bila kupoteza mchezo toka mwezi Februari huku wakimaliza katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa EPL. Ole Gunnar Solskjaer ambaye alikuwa na wakati mgumu katika kupanga kikosi imara, alitumia kikosi kimoja kwa michezo 5 ya mwisho na hivyo wachezaji hao kuchoka sana kutokana na muda mfupi waliotumia kati ya mechi na mechi.
Kuelekea katika hatua ya mtoano kwenye michuano ya Europa. Solskjaer anakila sababu ya kuwatumia wachezaji ambao hawajatumika sana katika michezo ya Ligi Kuu – EPL. Lengo likiwa ni kuwapumzisha baadhi ya nyota wake na kuwapatia nafasi wachezaji wengine.

Daniel James, Odion Ighalo, Juan Mata, Scott McTominay, Fred, Lingard, Andreas Pereira na Sergio Romero ni kati ya wachezaji ambao Ole Gunnar Solskjaer amekuwa akiwatumia sana kwenye mashindano haya [Europa] ikilinganishwa na EPL.
Japokuwa McTominay na Fred walipata nafasi ya kuonesha uwezo wao kwenye michezo ya EPL, ujio wa Bruno Fernandez na kurejea kwa Paul Pogba ambaye alikuwa majeruhi, kumewafanya wachezaji hao [McTominay na Fred] kukaa benchi kwa muda.
Kutokana na muda wa kuanza kwa msimu mpya wa EPL kuwa karibu sana [Septemba 12], ni dhahiri kwamba vilabu vinavyoshiriki michuano ya ulaya – UEFA na Europa vinakila sababu ya kufanya mabadiliko ya vikosi vyao katika michuano hiyo.

Solskjaer anafaida ya kuwa na kikosi kipana chenye wachezaji wenye uzoefu na ambao wameshatumika zaidi kwenye michuano hiyo. Pia, uwepo wa vijana chipukizi kama James Garner, Tahit Chong, Laid na wengineo ni msaada mkubwa kwa Solskjaer na benchi la ufundi la Manchester United.
United wanarudi katika michuano hii wakikutana na LASK ambayo walipoteza kwa Man United [5-0]. Hii ni faida kwa United ambao ni kama wanakamilisha ratiba hii na kuangazia zaidi hatua ya robo fainali.

Vyombo vya habari mbalimbali nchini Uingereza viliripoti taarifa ya kuongezwa kwa muda kwa timu zinazoshiriki Michuano ya Ulaya. Endapo timu shiriki zitacheza mpaka hatua ya fainali – Agosti 21 (Europa), zitaongezewa muda wa siku 7 zaidi ya timu zingine kunako EPL kwa ajili ya mapumziko na kujiandaa kuanza msimu mpya.
Wakati Manchester United na Wolverhampton Wanders wakipambana na Europa nchini Ujerumani. Manchester City na Chelsea wao watakuwa wanacheza michuano ya UEFA itayochezwa Ureno. City wakivaana na Real Madrid, wakati Chelsea wakikipiga dhidi ya Bayern Munichen.
Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.


Antony Luseno
Manager wa united inafaa afanye wonders katika kombe hili
aisha
Manchester united wako vizuri safari hii ni lazima wapate kombe
Tatu
Man wanatakiwa kukaza ili kufika malengo
Magdalena
United itapendeza wakikaza buti kutimiza malengo
Ester jackson
Mambo yaanze tu jamani ninasubiri kwa hamu kubwa sana
Zeiyana
Kila lakheri man u kwenye mashindano ya Europa.
Dorophina
Msimu huu man u wanaweza wakafikia malengo yao ya kubeba kombe
Sauda
Aminia Man U, tunatarajia ushindi
Salma ngende
Kila la her man u
Furahav
Man u bado iko vizuri
Latifa juma mohamed
Man u jeshi kubwa lazima watafanya maajabu.
Lydia Emmanuel Magoti
Man U awakubali kushindwa mahangamizi yanaenderea lazima wapambane wachukue kombe
Gabriel
Wajipange sana maana sisi tumewaachia wao FA linatutosha kabisa
Hv a good news 👍
felister
kila la kheri man u
Fatuma kasomo
Man kila la heri
Issa
United itapita round hii amna wa kumzuia
Ernest
Man U hawakosi sababu hawa wakitolewa huko utasikia tumechezesha kikosi B
Hope mwaikuka
Pambanen man u
Shafii
Man u ninaimani watavuka kikwazo hiki maaana kwa sasa nguvu zao zitakua hapo tu maana nafasi ya kucheza club bingwa msimu ujao wanao na wachezaji wana molari Kama zote za kuwa thibitishia wana man u kwamba walistahili kumaliza nafasi nzuri kwenye ligi ya uingereza na sasa wasubili makubwa kwa msimu ujao ila mchezo wa mpira unamambo mengi Sana lolote linaweza kutokea cha msingi tusubili nini man u watafanya.
Theonestina
Kila la kheri man u
farida ahmadi
Manchester United msituangushe mashabiki wenu tunasubiri kwa hamu kuona kivumbii kwenye Europa
Amiri Kayera
Kazi kwao man u
Sabrina
Man u nawatakia kila la kheri
Mwanahamisi
Kila la kheri man u
Samiah
Kazeni buti Man
Venerose
Kila la kheri man u
Rehema
Safi sn
Nasra
Man U iko vema sana
Caroline
Apa kazi ipo
Mwajumah
Man u naona wamejipanga vizur safar hii wanaweza kufika mbali
warda
Man U wako poa sana#Meridianbettz
Fatina mfingi
Kazi ipo
Khadija
Man u wapo poa sana#meridianbettz
Sadick
Man U inaweza kuchukua ubingwa wa Europa msimu huu#meridianbettz
Saupha mohamed
Man u IPO vizurii
Devotha
Kila la heri man united
David Pere
Man U wanalitaka kweli hili kombe