Mukwala Ana Mipango Yake Simba

Mshambuliaji wa Simba SC Steven Mukwala hesabu zake ni ndefu kwenye kikosi hicho ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids katika mechi za ushindani.

 

Mukwala Ana Mipango Yake Simba

Mukwala ameweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kuona timu hiyo inapata matokeo chanya kwenye mechi ambazo wanacheza ndani ya uwanja msimu wa 2024/25.

Mshambuliaji huyo anaingia kwenye orodha ya wakali wakucheka na nyavu Bongo akiwa katupia mabao 12 na kutoa pasi tatu za mabao akihusika kwenye mabao 15 ndani ya kikosi cha Simba SC ambacho kimefunga mabao 63.

Katika michuano ya kimataifa msimu huu, Mukwala alicheza michezo tisa na kufanikiwa kufunga bao moja la muhimu kwenye mchezo wa kufuzu kuingia hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya El Masry.

 

Mukwala Ana Mipango Yake Simba

Kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars uliochezwa Uwanja wa KMC, Mukwala alifunga bao pekee la ushindi lililoipa pointi tatu Simba SC kwenye mchezo huo na alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

“Kazi ni kubwa kwenye mechi ambazo tunacheza na mpango ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya inawezekana na tunashirikiana na benchi la ufundi kuona kwamba matokeo yanapatikana.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mukwala Ana Mipango Yake Simba

 

Mchezo ujao kwa Simba SC ni Juni 15 2025 dhidi ya Yanga SC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa huku Yanga SC ambao ni wenyeji wakibainisha kwamba hawapo tayari kwa mchezo huo namba 184 mpaka matakwa yao manne waliyoyatuma kwenda bodi ya ligi yatimizwe. Mchezo huo ulipangiwa tarehe mpya mara baada ya kuhairishwa awali mnamo Mei 08 2025 kutokana na sintofahamu iliyotokea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.