Matumaini ya Novak Djokovic Yanasalia French Open

Novak Djokovic ametangaza kuwa hatashiriki michuano ya Indian Wells Masters na Miami Open kutokana na kigezo cha chanjo ya Covid19 kuwa kigezo cha kushiriki kwake.

Mshindi huyo mara 20 wa Grand Slam aliondolewa Australia kabla ya michuano ya Australian Open mwezi Januari kwa sababu hii hii na akasisitiza kuwa atakuwa tayari kukosa michuano mingine mikubwa kutokana na msimamo wake.

Novac Djokovic
Novac Djokovic

Djokovic aliitwa kwenye orodha ya washiriki wa mashindano ya Indian Wells mwaka huu, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 sasa amethibitisha kuwa hataweza kucheza, huku Marekani ikiwazuia watu ambao hawajachanjwa kuingia nchini.

“Ingawa niliorodheshwa kiotomatiki kwenye droo ya @BNPPARIBASOPEN na @MiamiOpen nilijua nisingeweza kusafiri” Novak Djokovic alisema kupitia ukurasa wake wa tweeter.

 

“CDC imethibitisha kuwa kanuni hazitabadilika kwa hivyo sitaweza kucheza Marekani. Kila la kheri kwa wale wanaocheza katika mashindano haya makubwa.”

Hivi majuzi Djokovic alifika robo-fainali ya Mashindano ya Tenisi ya Dubai mwezi uliopita lakini ametiwa nguvu katika azma yake ya kushiriki michuano ya French Open mwaka huu na kutetea taji lake la 2021 baada ya kubadilika kwa masharti ya chanjo Ufaransa.


 

VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe