Mkataba wa Paulo Dybala na Juventus unamalizika mwishoni mwa msimu huu. Kuna taarifa kuwa tayari amefanya maamuzi kuhusu wapi anataka kuelekea. Hii ni baada ya kubainika kuwa staa huyu hatasalia Turin.

Atletico Madrid na Barcelona wote walikuwa wametajwa kuhitaji huduma ya Paulo Dybala. Kwa mujibu wa Gazzetta dello Sport kama ilivyoainishwa na Marca fowadi huyo hataondoka Italia.

Taarifa inataja kuwa nyota huyu atajiunga na wapinzani wakali wa Juventus Internazionale.

Dybala atasaini mkataba wa miaka minne pale San Siro wenye thamani ya €6m kwa mwaka.

Dybala ameichezea Juventus mechi 289, akichangia mabao 114 na asisti 48. Ameshinda Scudetto mara tano, Coppa de Italia mara nne na Supercoppa Italiana mara tatu.

Dybala anatumaini kwamba uhamisho wake katika majira ya joto unaweza kumkuza kwenye kikosi cha Argentina cha Lionel Scaloni kuelekea Kombe la Dunia la 2022. Argentina wakiongozwa na Lionel Messi wataelekea Qatar.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa