Kirusi cha Variant Omicron kinaendelea kuwa gumzo duniani. Pep Guardiola hana tatizo na namna EPL inavyoendelea nyakati hizi.
Man City, Chelsea, Arsenal na Newcastle ndio vilabu pekee vya EPL ambavyo havijapata msukosuko wa michezo yao kughairishwa. Kuelekea wiki ya 19, baadhi ya vilabu tayari vina michezo 3-4 pungufu kwa msimu huu.
City watakua uwanjani wikiendi hii kuchuana na Leicester City. Pep Guardiola anaona kwake kila kitu kipo sawa. Anaheshimu mamlaka yaliyowekwa kwa EPL na hivyo, vyovyote uongozi wa Ligi utakavyoamua, Manchester City itatekeleza.

Sanjari na hayo, Guardiola anasisitiza, kitu muhimu kwake siku zote ni furaha kwa wachezaji wake. Kama mchezaji hana furaha kuwepo Man City, Pep haonishida kumruhusu mchezaji husika kuondoka.
Msimamo huu wa Pep unatokana na Ferran Torres kuomba kuondoka klabuni hapo na kwenda Barcelona. Kwa hali ilivyo hivi sasa, usajili huu umekamilika, ni suala la muda tu kabla Barca na City hawajatoa uthibitisho wa Torres kutua Camp Nou akitokea Etihad Stadium.
Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.


