Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi sababu ya kumuza aliyekuwa nyota waklabu hiyo ambae kwa sasa amejiunga na klabu ya chelsea Raheem Sterling baada ya winga huyo kukubali kuwa alikuwa na hasira kwenye uhamisho wake.

Pep Guardiola ametetea uamuzi wake wa kumuuza winga huyo baada ya hivi karibuni kwenye mahojiano na kituo cha Skysport kunukuliwa akisema: “Kila mmoja anataka kujihisi kutakiwa, Mpira hauna utofauti. Unapocheza kwa moyo wako wote, unakosa kushiriki siku za kuwaliwa watoto wako, na kisha unakuwa utendewi vizuri inakatisha tamaa.

Pep Guardiola, Pep Guardiola: Ukihitaji Kuondoka Tutakusaidia, Meridianbet

“Kuna muda unakuwa hasira, kinyongo  lakini imekwisha, yashapita na sasa naweza kujikitwa kwa maswala ya kipindi hiki.

Pia alizungumzia kuhusu kuondokwa kwenye majira ya kiangazi, Sterling alisema: “Kutokuwa na maelewano, mkataba kuelekea mwishoni. Ilikuwa aibu kuona vitu vinaelekea mwishoni kumalizika sababu nilikuwa na muda bora sana pale.”

Baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kuzungumza, Pep Guardiola aliulizwa kuhusu kuondoka kwa wachezaji kwenye dirisha hili kama kocha alielezea anavyodhani kuwa na wachezaji wasio na furaha.

“Kama ukimlazimisha mchezaji mmoja abaki wakati hataki kubaki unawezaje kupata ubora wake? Haiwezekani.

“Sitaki kumuondoa mchezaji yoyote sasa. Nakipenda kikosi changu nilichonacho. Najisikia amani kufanya mazoezi nao sababu baada ya miaka sita, saba tunajuana vizuri sana. Katika vipanda vibaya  najua jinsi wanavyokuwa , wako vizuri kiuweledi.

“Ningependa tukae wote pamoja lakini muda huo huo dirisha la usajiri linafika tamati kati ya siku 10 -15 na kama mchezaji anataka kuondoka basi tutamtafutia suruhu. Ipi , sijui lakini tutamtafutia.”

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa