Platini,Blatter Kushtakiwa Tena.

Rais wa zamani wa Uefa Michael Platini na rais wa zamani wa Fifa Sepp Blatter wako mashakani kushitakiwa tena baada ya mwanasheria mkuu wa nchi ya Uswisi kukataa rufaa juu ya viongozi hao kuachiwa.platiniViongozi hao wa zamani wa mpira walifutiwa mashtaka yao yaliyokua yakiwakabili katika mahakama ya uhalifu wa kishirikisho huko Bellinzona na matokeo hayo yalitangazwa mwezi Julai mwaka huu.

Platini na Blatter walishtakiwa kwa ulaghai na makosa mengine na mamlaka ya Uswizi kuhusiana na malipo ya faragha ya milioni 2 ya Uswizi iliyotolewa na Blatter kwenda kwa Platini mwaka 2011. Kwa Blatter yeye alishatakiwa kwa makosa ya ulaghai,matumizi mabaya ya fedha, usimamizi mbovu wa jinai na kughushi hati.platiniHuku rais wa zamani wa Uefa yeye akishtakiwa kwa udanganyifu, kushiriki katika matumizi mabaya ya fedha,usimamizi mbovu wa ofisi na kughushi hati.

Viongozi hao wa zamani walikana mashatka hayo na mahakama ikakubaliana nao lakini kuna hatihati ya kushtakiwa tena kwani waendesha mashtaka hayo hawakuridhishwa na hukumu iliyotoka huku wakiongozwa na mwanasheria mkuu wa nchi ya Uswizi.


 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.