Mgunda Tunahitaji Ushindi Kwenye Derby.

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Juma Mgunda amesema malengo yao kama timu ni kwenda kushinda mchezo wa derby siku ya jumapili Oktoba 23 utakaopigwa katika uwanja wa taifa Benjamin Mkapa.

Klabu ya Simba na Yanga zitakutana siku ya jumapili katika mchezo wa derby ya Kariakoo ambao huzikutanisha timu hizi kongwe zaidi Tanzania ambapo mchezo huo huteka hisia za mashabiki wa mpira Tanzania.mgundaKocha Mgunda amesisitiza kua anatambua kua mchezo dhidi ya Yanga utakua mgumu lakini lengo kubwa zaidi kuelekea mchezo huo ni kupata matokeo mazuri katika mchezo huo na kutowaangusha mashabiki wa timu hiyo.

Mgunda ameleeza kua hawataenda kwa mazoea kucheza mchezo huo wao huku wakiendelea kuandaa timu ya ushindi kuelekea jumapili.mgundaSimba haijashinda mchezo wowote wa ligi kuu dhidi ya Yanga tangu mwaka 2019 huku mashabiki wa timu hiyo wakiwa na hamu ya kupata matokeo dhidi ya watani zao kwa kiwango kikubwa huku imani yao kubwa ipo kwa kocha huyo ambaye hajapoteza mchezo wowote toka aichukue timu hiyo.

Acha ujumbe