Mlinzi wa kimatafa kutoka Ujerumani anayekipiga kwenye klabu ya Chelsea Antonio Rudiger anatarajia kujiunga na klabu ya Real Madrid mwishoni mwa msimu kwa uhamisho huru kwenye majira ya kiangazi.

Rudiger mwenye umri wa miaka 29, anatarajia kusaini kandarasi ya miaka minne  na miamba ya  Los Blancos, Klabu za  Manchester United, Barcelona na Paris Saint-Germain nazo zilikuwa zinavutiwa na huduma yake.

Rudiger

Siku ya jumapili kocha wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel alithibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo kwenye dimba la Stomford Bridge, kutokana na kuwekewa kwa vikwazo dhidi ya mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich ni moja ya sababu kuu ambayo ilipelekea Chelsea kushindwa kumuongezea mkataba wake.

Rudiger ameitumikia kwa miaka mitano sasa klabu hiyo baada y kusajiri kwa ada ya uhamisho wa £29 million akitokea nchini italia kwenye klabu ya Roma, muda aliutumia akiwa na chelsea amefanikiwa kushinda FA Cup, Europa League 2019, ligi ya mabingwa Ulaya 2021 na kombe la dunia la vilabu na UEFA super cup.

Msimu huu Rudiger msimu huu ameichezea Chelsea michezo 47 kwenye mashindano yote, huku kwenye timu yake ya taifa ya Ujerumani amechezea michezo 50 mpaka sasa.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa