Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) imesema kwamba hakuna mchezaji aliyeruhusiwa kucheza ligi bila ya kuwa na mkataba, hivyo kauli ya Bernard Morrison kuwa alicheza mechi mbili bila mkataba ni uongo.

Kamati ya katiba, sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF imesema kwamba hakuna mchezaji aliyeruhusiwa kucheza ligi kuu bila ya kuwa na mkataba.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Elius Mwanjala, ametoa kauli hiyo akitolea ufafanuzi alichokisema mchezaji Bernard Morrison kuwa aliitumikia Yanga katika michezo miwili bila ya kuwa na mkataba.
Mwanjala amesema kauli ya Bernard Morrison ni ya uongo kwa kuwa utaratibu wa wachezaji wote kucheza Ligi Kuu unafahamika, ni lazima awe na mkataba ili kupata usajili na uhalali wa kucheza ligi kuu.
Kuhusu masuala ya mkataba wa Morrison, Mwanjala amesema wanasubiri kupokea baadhi ya nyaraka kutoka Yanga ili kufahamu uhalali wa mkataba wa miaka miwili ambao mchezaji anakana kuwa hajausaini.
Hata hivyo kamati hiyo imekiri kuipokea mikataba ya miezi sita na miaka miwili ya mchezaji huyo lakini wanasubiri kikao cha mwisho kuzipitia nyaraka zitakazowasilishwa na Yanga.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amesema wanaendelea kushughulikia malalamiko ya Yanga ambao waliyafikisha katika kamati yao juu ya moja ya klabu nchini kutumika kumrubuni mchezaji wao Bernard Morrison kiasi cha kuukana mkataba wao.

Vilevile kamati imesema itatoa hukumu ya pamoja dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, ambaye amelalamikiwa kuleta taharuki ndani ya Wekundu wa Msimbazi kwa kutangaza katika vyombo vya habari kuwa wamekamilisha mazungumzo na kiungo wao Clautius Chama, kinyume na utaratibu.


Omary lukumbi
Jambo hili si sawa kabisa jambo aliweza kuiyumbisha yanga kwa kipindi fulan kwa kukosa huduma yake
Amiri Kayera
Ni vizur San TFF kusimamia ilo
Theckla
Sidhani Kama ni sahihi
Theonestina
😀😀😀watani zangu wamefulia
neema hassan
Asante kwa taarifa#meridianbettZ
Njiku
Safii
Shafii
Ishu ya Morison ni ngumu Sana inatakiwa tamko litoke kwa viongozi nn tatizo kuhusu mchezaji Huyo na wamefikia wapi hadi sasa.
Gabriel
Yanga wamegundua kuna kitu kinaendelea baina ya kiungo mshambuliaji wao, Bernard Morrison na baadhi ya watu wa Simba. Morrison hakuwepo kwenye kikosi cha Yanga kilichowavaa Mwadui juzi mjini Shinyanga, baada ya kuwazimia simu viongozi siku ya kuondoka Ijumaa asubuhi huku akiwaambia wenzake kwamba, bado ana hofu na virusi vya corona. Awali, nyota huyo aliyekaa kwenye mioyo ya mashabiki wa Yanga baada ya kuwafunga Simba, aligoma kusafiri kwa basi na wenzake lakini hata alipopewa tiketi ya ndege akaingia mitini. Mmoja wa vigogo wa Yanga amesema kuna habari wamezisikia kuwa kuna kigogo mmoja wa Simba alimpa mchezaji huyo kishika uchumba cha dola 10,000 (Sh23milioni). Mkataba wa miezi sita wa Morrison na Yanga unaelekea ukingoni na tayari walishasaini mkataba mwingine wa miaka miwili zaidi ambapo tayari mkataba huo upo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ingawa inadaiwa kwamba, haujakamilika katika baadhi ya makubaliano na hapo ndipo Mghana huyo ameanza kuwashika pabaya. Kwa upande wake Morrison, amesema kuwa ataungana na kikosi Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania na kujitetea kwamba hakuweza kujiunga na kikosi Shinyanga kwa kuwa alikuwa bado na maumivu kwenye mguu hivyo aliona ni bora atulie kwanza maumivu yatulie.
Issa
Safi sana
Furahav
Morrison anazingua,afungiwe mechi 10.
Edgar
Safi kabisa
Franky
Good nwes..
Hamidu
Asante kwa update za michezo
Hope mwaikuka
Duh
Frank Patrick
Bongo nyoso
Neema juma
Ni habari nzuri
Rehema
Asante meridianbet kwa taarifa
Fatuma kasomo
Safi tff
Caroline
Kwani mkataba wa Morrison una shida gani
warda
Mmmm!! Huyu nae wanamkuza kila siku kumpa bichwa#Meridianbettz
Mwanahamisi
Safi sana
Asia Abdy
Hij saf sana
Johnmary joel
Hongera #meridianbett
Magdalena
Duh hii balaa
Dorophina
Morisoni anahangaika km anataka kuama timu si aseme tu kuliko maneno mengi yy anadhani bila yy yanga haitoweza kufanya chochote
David Pere
Tff wanatia aibu kweli Yani muda wote huo Ndio wanajua hivi karibu ,wakati mwingine wawe wanajiongeza
felister
safi
Tatu
Safi sana
Angelina
Gudupdate
JULIANA
TFF iko sawa kabisa
Genia Sikaluzwe
Saf Sana
isha
Hii sio sahihi kabisa
Ester jackson
Hapa kuna kitu kinaendelea baina ya mchezaji wa yanga Morrison na majirani wekundu wa simba haiwezekani kila siku jipya linaibuka kwa ajili yake sasa wameguuka eeti yanga wanamtaka mchezaji wa simba chama ili iweje ikiwa bado mkataba wake haujaisha simba .
Samira
Morrison anazingua sana yaani anataka kuwa juu ya timu yenyewe hana nidhamu
Evaluziga
Morrison anazingua mtoeni kabisa analinga achaneni nae
Leonard
Tff watende haki
Salma
Mh! Hapa kuna kitu nyuma ya pazia
Khadija
mh!!hapa kuna kitu#meridianbettz
Saupha mohamed
Siyo poa
Flomena
Sizani Kama Morrison anafanya vizuri
devotha
asanteni sana kwa taarifa maana Morrison alitaka kuvuruga vichwa vya mashabiki yanga
Samiah
Morrison hafanyi vzr
Ernest
Mpira wa Bongo una mambo sana
Fatina mfingi
Hatar
Lydia Emmanuel Magoti
Safii Sana TFF kuingilia Kati ilo sakata