Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah anawaza kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote ndani ya klabu hiyo katika michezo ya ligi kuu ya Uingereza ili kuivunja rekodi ya gwiji Robie Fowler.

Mohamed Salah amekua kwenye kiwango kikubwa ndani ya klabu ya Liverpool tangu amejiunga ndani ya klabu hiyo na kuelekea mchezo wao dhidi ya klabu ya Manchester United mchezaji huyo anahitaji mabao mawili tu kuvunja rekodi ya Robie Fowler anaeongoza kwa mabao ya ligi kuu ya Uingereza akiwa na mabao 128 huku Salah akiwa na mabao 126.salahMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Egypt amefanikiwa kua na ubora mkubwa ndani ya klabu ya Liverpool, Huku akifanikiwa kufunga walau mabao 20 kwenye kila msimu ambao ameitumikia klabu hiyo huu ukiwa msimu wa saba ndani ya Liverpool.

Mohamed Salah amekua na rekodi nzuri dhidi ya klabu ya Manchester United msimu uliomalizika akifanikiwa kuifunga klabu hiyo mabao matano katika michezo miwili waliyokutana, Hivo inawezekana mchezaji akapata mabao yake mawili kupitia mchezo huo.salahMshambuliaji Mohamed Salah licha ya kufikisha mabao 20 msimu huu kwenye michuano yote lakini ameonekana kua chini ya kiwango kidogo, Huku klabu yake ya Liverpool pia ikiwa inachechemea hii inaelezwa kua moja ya sababu ya mchezaji huyo kutofanya vizuri ni kutokana na klabu yake pia kutofanya vizuri.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa