Leroy Sane atawapa furaha sana Bayern Munich, hii ni kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Schalke Joel Matip.

Bayern Munich mwezi uliopita walikamilisha dili ya muda mrefu ya uhamisho wa Sane kwa makubaliano ya kitita cha €60m akitokea kunako klabu ya Manchester City.

Uhamisho wa Sane ulitangazwa katikati miamba hiyo ilipokuwa imeshashinda taji lao la nane la Bundesliga na kumaliza mashindano ya DFB-Pokal kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Bayer Leverkusen.

Mlinzi wa Liverpool Matip anaamini Sane atakuwa na muunganiko mzuri na wachezaji wa Bayern ingawa anahofia kuongezeka kwake kutaleta ugumu wa kiushindani ndani ya Mabingwa hao wa Ujerumani.

Sane, Sane Atawapa Raha Bayern Munich – Matip., Meridianbet

“Namjua Sane vizuri sana, Ni mchezaji bora Leroy katika hali isiyo tarajiwa ataleta furaha Bayern Munich,” Matip aliiambia Die Welt.

“Leroy ni mchezaji ambaye anaweza sana kuisaidia timu.”

Kufuatia kuwa na majeraha ya mguu ilimfanya asihusike na timu ya Manchester City msimu walio washuhudia Liverpool wakinyanyua ndoo msimu huu tangu walipo fanya hivyo mwka 1990.

Matip aliulizwa kama ubingwa wa Premier League ni mkubwa kushinda ule wa mwaka uliyopita wa Champions League kwa Liverpool, alisema “ndiyo ilikuwa kama hivyo, lakini yote yamefanywa na klabu, lakini huu wa Premier League ni muhimu kwani ni miaka 30 imepita ilikuwa ni shauku kubwa kwa mashabiki kusubiri kipindi chote.

“Kwa kuongeza, kila klabu ina shauku yake. Manchester City ubingwa wa Champions League unathamani kubwa zaidi.”

Jurgen Klopp akiwa Borussia Dortimund mwaka 2012 ndiyo ilikuwa timu ya mwisho kuwapiku Bayern Munich na kutwaa ubingwa wa Bundesliga na Matip amesifu mafanikio ya ya Meneja huyo tangu atimkie Anfield, ambako pia amefanikiwa kushinda mataji mbalimbali kama UEFA, Super Cup na Club World Cup.

 


 

Kuna ofa kibao unazaofaidi ikiwa unabashiri na Meridianbet. Jiunge sasa kufurahia ofa zetu

Bonyeza HAPA Kujiunga.

48 MAONI

  1. Bayern nina imani watafurahi na usajili huo kwani Sane ni nyota sana kwa sasa ingawa alikua benchi takribani mwaka mzima kutokana na majeraha

  2. Sane uwezo wake ulikuwa mkubwa city kiwango alichokionyesha anatkiwa akionyeshe akiwa munich ingawaje mazingira na falsafa za kocha zitampa shida mwanzoni

  3. Sane ni mchezaji mzuri sana, amekuwa imara sana ndani ya kikosi cha Mancity natumaini atafanya vizuri katika club ya Bayern.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa