Klabu ya Simba SC imetangaza kuachana na beki wa kati raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa msimu huu mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa mwezi huu.
Baada ya kuitumikia Simba kwa misimu minne, Pascal Wawa hatakuwa sehemu ya Kikosi cha Simba msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa Juni 2022.
Beki huyo raia wa Ivory Coast aliyejiunga na Simba mwaka 2018 akitokea Al Merrikh ya Sudan ambayo ilimsajili kutoka Azam FC, atacheza mchezo wake wa mwisho na Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar Juni 23, 2022.
Wawa ni mchezaji wa tatu kuagwa na Simba SC kwa msimu huu baada ya Bernard Morrison na Rally Bwalya kutangazwa kuondoka ndani ya timu hiyo.
‘Merci beaucoup Pascal Wawa’
ALIYA’S WISHES
Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.
Ubashiri wa Meridian | Simba Kuwashukuru Mashabiki Wake
[…] Simba SC Yamuaga Rasmi Pascal Wawa. […]