French Open: Mashabiki Wapunguzwa Mpaka 1,000

Kuelekea Mashindano ya French Open, idadi ya mashabiki imepunguzwa kutokana na sheria mpya za kujilinda na COVID 19.

Awali, ilipangwa mashabiki takribani 11,500 wangeruhusiwa kuingia uwanjani na wiki iliyopita idadi hiyo ilipunguzwa mpaka 5,000. Tamko jipya limepunguza idadi hiyo na kuwa 1,000 kwa siku kufuatia serikali kutangaza utaratibu mpya kama sehemu ya kujilinda na COVID 19.

Mashindano ya French Open kikawaida yanafanyika mwezi Mei-Juni na mashabiki 35,000 wanakuepo uwanjani kushuhudia michezo inayochezwa kila siku. Kutokana na mlipuko wa COVID19, mashindano hayo yalisogezwa mbele na sasa yataanza jumapili wiki hii.

French Open
Kombe la French Open 2020

Shirikisho la mchezo wa tenesi nchini Ufaransa limesema, “Tangu kuanza kwa hili janga tunalolipitia kama nchi, shirikisho limekuwa likifanya kazi kwa ukaribu zaidi na idara za serikali, tukipanga ni kwa namna gani tunaweza kuendesha mashindano haya katika hali hii.

“Tunasikitika kwa hizi sheria mpya.”

Rafael Nadal atashiriki mashindano mwaka huu akiwa analisaka taji la 13 kwenye French Open. Endapo Nadal atafanikiwa kutwaa taji mwaka huu, atakuwa sawa na Roger Federer kama wachezaji wenye mataji 20 ya Grand Slam.


 

FURAHIA KASINO YA MTANDAONI

Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.

Cheza Sasa

30 Komentara

    duuh corona inatunyima uhondo

    Jibu

    Hii bado ni hataree kuhusu corona. Ila kwa ajili ya afya za wengi inabidi tukubaliane na hali yenyewe

    Jibu

    Covid 19 imetuharibia kila pembe jamani mungu tuu atulinde

    Jibu

    Sio mbaya maana tulipo toka sio tulipo sasa bora watu waingie uwanjani kuangalia michezo

    Jibu

    Bado sio mbaya

    Jibu

    Vzuri kujikinga na corona

    Jibu

    Coron inatunyima raha

    Jibu

    Doooo so sad

    Jibu

    Corona imevuluga Mambo na kutukosesha raha jmn

    Jibu

    Covid 19 hatari Sana inatukosesha burudani

    Jibu

    Bora ata ivyo kuliko kutokuwepo kabisa

    Jibu

    Corona bdo ipo kujikinga lazima

    Jibu

    Waendelee kuchukua tahadhari Corona is real jmn

    Jibu

    Bola ataivyo kuliko kutokuwepo kabisa mashabiki

    Jibu

    Coronavirus sio poa

    Jibu

    Corona nomaa

    Jibu

    Corona imeleta balaa

    Jibu

    Vzuri kujikinga na corona

    Jibu

    Inabid tahadhari ichukuliwe dhid ya korona

    Jibu

    Adah Corona hii jaman

    Jibu

    Sio mbaya kuliko kutokuepo kabisa

    Jibu

    Jambo zuri kwa ajili ya usalama wa afya za mashabiki

    Jibu

    Duuh corona hii

    Jibu

    Balaa zito corona inatunyima , inatukosesha Mambo mazuri lkn kwa watu 1000 uwanjani sio mbaya Sana.

    Jibu

    Balaa zito corona inatunyima , inatukosesha Mambo mazuri lkn kwa watu 1000 uwanjani sio mbaya Sana.

    Jibu

    tahadhari ni muhimu kuliko tiba huu ugonjwa si wakuchukulia masihara sana

    Jibu

    Sio mbaya kwa watu hao wanatosha kabisa kuleta amsha amsha uwanjani

    Jibu

    Siyo mbaya kuliko kutokuwepo kabisa

    Jibu

    Covid 19 noma sana hiiii janga la dunia

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.