Tetesi zinasema, Manchester City na Juventus zimekubaliana kuhusu uhamisho wa mshambuliaji mreno Cristiano Ronaldo, 36, kujiunga na klabu hiyo. Ada ikiwa kati ya £21m-25m, City watampa mkataba wa miaka 2.
Tetesi zinasema, Wolverhampton Wanderers imekataa ofa ya mkopo kwa ajili ya winga wake raia wa Hispania Adama Traore, 25, kutoka Tottenham Hotspur, wakitaka kumbakiza.
West Ham United inamnyemelea mshambuliaji wa CSKA Moscow na Croatia Nikola Vlasic, 23, wakiendelea kutafuta mbadala wa kiungo mshambuliaji wa Manchester United na England Jesse Lingard.

Tetesi zinasema, Watford imeanza mazungumzo na Tottenham kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo mfaransa Moussa Sissoko, 32.
Paris St-Germain inaendelea kusaka wachezaji akiwemo kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, wakati wakijiandaa kumuuza Kylian Mbappe.
Tetesi zinasema, Real Madrid imeongeza dau lake kufikia £145m kwa ajili ya mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Mbappe, 22, baada ya dau lake la awali la £137m kukataliwa.
Manchester United imemkosa winga wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 Noni Madueke, 19, baada ya nyota huyo kusaini mkataba mpya na klabu yake ya PSV Eindhoven.
Tetesi zinasema, Chelsea wanakaribia kabisa kumsajili mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 22, katika uhamisho utakaogharimu £42m.
Tetesi zinasema, Tottenham imeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Juventus na Marekani Weston McKennie, 22 uhamisho utakaogharimu £40mil.

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta ametupilia mbali uwezekano wa nahodha na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kuondoka klabuni hapo.
Tetesi zinasema, Everton inamtaka mshambuliaji wa Brighton mfaransa Neal Maupay, 25.
Manchester United inataka kusajili kiungo kabla ya dirisha la usajili kufungwa, lakini itawapasa kusubiri kuona kama wanaweza kumpata kiungo wa England na West Ham Declan Rice, 22.
Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.



Sarah
Ziko vizuri tetesi