Tetesi zinasema, meneja wa Manchester City Pep Guardiola anaitaka klabu hiyo kumsajili kiungo wa kati wa Leeds na England Kalvin Phillips, 25, msimu ujao.
Barcelona inamlenga mchezaji wa RB Leipzig Dani Olmo , huku Manchester United , Juventus na Bayern Munich pia zikiwania saini ya winga huyo mwenye umri wa miaka 23.
Tetesi zinasema, Beki wa Leicester City na Ufaransa Wesley Fofana, 20, anasema kwamba Real Madrid ndio klabu kubwa duniani na kwamba ni ndoto yake kuichezea klabu hiyo.

Tetesi zinasema, Everton ilishindwa kumuuza kiungo mchezeshaji wa Colombia James Rodrigues kutokana na mshahara wa £250-000- kwa wiki.
Baadhi ya klabu za Uingereza zinamnyatia mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 21 , licha ya mchezaji huyo kutia saini kandarasi ya muda mrefu na Real Sociedad. Arsenal na Chelsea awali zimeonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo.
Tetesi zinasema, Tottenham Hotspur imefungua mazungumzo na Ajax kuhusu uwezekano ya kumsajili beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 20 Jurrien Timber.

Barcelona inapanga kufanya mazungumzo na ajenti wa Ousmane Dembele kuhusu kuongeza kandarasi ya mshambuliji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24, lakini hakuna mkutano uliofanyika kufikia sasa.
Mshambuliaji wa Serbia 21, Dusan Vlahovic, alivivutia vilabu vya Tottenham na Atletico Madrid mwisho wa msimu uliopita , yupo katika mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba wake na klabu ya Florentina.
Kiungo mchezeshaji wa Ufaransa Houssem Aouar, 23, amepinga mazungumzo yanayomuhusisha yeye na klabu ya Arsenal na anasema anataka kuisadia Lyon kufuzu katika kombe la klabu bingwa Ulaya.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


