Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Newcastle United wanazidi kuwa na uhakika wa kumsajili beki wa Uingereza Kieran Trippier, 31, kutoka Atletico Madrid mwezi ujao.

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel anasema atawasiliana na Pierre-Emerick Aubameyang baada ya mshambuliaji huyo wa Gabon, 32, kuvuliwa unahodha wa Arsenal.

Tetesi zinasema, Barcelona wanajiandaa kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21.

 

Baada ya Mbappe ni Rudiger, Vita ya Madrid na PSG

Mlinzi wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, 28, ambaye amebakiza miezi sita katika mkataba wake, amethibitisha kuwa anafikiria kuondoka katika klabu hiyo kabla ya Thomas Tuchel kuteuliwa kuwa meneja mwezi Januari.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anasema mlinzi wa Uingereza Joe Gomez, 24, hataondoka na kujiunga na Steven Gerrard huko Aston Villa katika dirisha la uhamisho la Januari.

Kiungo wa kati wa RB Leipzig Amadou Haidara, 23, amechochea uvumi unaomhusisha na Manchester United baada ya kumsifu kocha wa muda wa klabu hiyo Ralf Rangnick.

Mshambuliaji wa Inter Milan Alexis Sanchez, 32, anaweza kurejea Barcelona kwa mkopo, huku mshambuliaji Luuk de Jong, 31, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Barca kutoka Sevilla, akihamia Inter.

 

Tetesi zinasema, Mlinzi Nat Phillips, 24, amekiri kwamba yuko tayari kuondoka Liverpool mwezi Januari kutafuta soka la kawaida.

Tetesi zinasema, Middlesbrough wako kwenye mazungumzo ya kusajili washambuliaji wawili kwa mkopo mwezi ujao.

Tetesi zinasema, West Ham ni miongoni mwa vilabu vya Ulaya vinavyotaka kumsajili mlinzi wa Argentina anayechezea Feyenoord Marcos Senesi, 24.


ANZA MSIMU WA SIKUKUU NA BURST THE BANK

Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.