Tetesi zinasema, Meneja mpya wa Manchester United Erik ten Hag anamlenga kiungo wa kati wa Ufaransa na Chelsea N’Golo Kante, 31, huku akitarajia kufanya mabadiliko Old Trafford.

Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 30, atakuwa akifuatiliwa na Bayern Munich ikiwa mshambuliaji wao wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski ataondoka msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Lewandowski, 33, amekubali kujiunga na Barcelona kwa mkataba wa miaka mitatu.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Barcelona Mfaransa Ousmane Dembele, 24, yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na Bayern Munich.

Kiungo wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, yuko tayari kuondoa takriban pauni milioni 6 kwenye mishahara ambayo haijalipwa ili kuhamia Manchester City.

Newcastle wamefanya mazungumzo ya awali na mshambuliaji wa Everton Dominic Calvert-Lewin, 25, lakini upendeleo wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ni kujiunga na Arsenal.

Arsenal wamekubali ada ya hadi euro 25m (£21.2m) kwa beki wa pembeni wa kimataifa wa Bologna na Scotland Aaron Hickey.

 

Pogba

Juventus wako tayari kumrejesha kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 29, katika klabu hiyo msimu huu wa joto. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

West Ham, Southampton na Brentford wanavutiwa na beki wa kulia wa Fenerbahce Mnigeria Bright Osayi-Samuel, 24.

Aston Villa wameungana na Crystal Palace na Brentford katika kinyang’anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Nigeria Joe Aribo, 25, anayechezea klabu ya Rangers.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa