Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kilifanikiwa kukata tiketi ya kuweza kusonga mbele kwenye michuano ya Euro 2020 baada ya kuibuka na ushindi mnono sana kwenye mechi yake. Kikosi hicho mbali na ushindi bado kilionesha kina changamoto katika ukomavu wake jambo ambalo linawaondoa kwenye ushindani.
Kikosi hicho kwa sasa bado kipo katika hatua za kujijenga kwa sababu wakongwe wengi wameweza kuachwa nje na kocha wa kikosi hicho tangu kiweze kupata matokeo mabovu kwenye michuano ya kombe la dunia. Hatua aliyoweza kuifanya kocha ni kupunguza wakongwe na kuanza kufunza vijana zaidi.
Ugumu unaokuja ni kwamba vijana wengi wanaozungumziwa ndani ya kikosi hicho bado hawana uzoefu wa kutosha kuweza kulisukuma gurudumu hilo mbele. Kwa sababu mara nyingi uzoefu huwa na mchango mkubwa sana hasa katika michuano mikubwa kama hiyo ambayo inakutanisha wazoefu.

Kroos ambaye ni kati ya wakongwe wachache waliobakia ndani ya kikosi hicho kwa sasa aliweka wazi kwamba bado wana kubwa la kufanya ndani ya kikosi hicho kwa sababu bado hawana ile kasi ya kuhitaji matokeo kwa haraka na baadhi ya maeneo bado yana changamoto katika kikosi chao hicho.
Anaamini kwamba bado wanahitaji maandalizi na mechi nyingi zaidi ili waweze kujiimarisha kwa nguvu ya ushindani kama wengine wanavyoonesha ukomavu. Hofu yake kubwa juu ya kikosi chao ni namna wanavyocheza kwa kuruhusu wapinzani wao kupata nafasi ya kuweza kuwashambulia kwa wakati mwingi.
Ujerumani Tamu Zaidi
Ujerumani inayokumbukwa ni ile ambayo ilikuwa inashinda magoli mengi kwa wakati mwingi wa mechi zake na kila timu iliyokuwa inakutana naye ilikuwa na sala yake juu ya mvua ya magoli ambayo ingeweza kuwakuta. Lakini kwa sasa kibao kimegeuka na wao ndio wamekuwa wahanga wa kuweza kupokea vipigo hivyo.
Ujerumani walipata ushindi huo mbele ya Belarus kwa jumla ya magoli 4 – 0 ambayo kwa hakika ilikuwa ni ushindi mzito kwao. Na safari yao imekuwa njema sana kwa sababu wataendelea kupambana kwenye michuano hiyo. Labda wasiwasi wa Kroos una kitu cha pekee ambacho amekiona, tuwape muda zaidi.


Povel tz
Noma sana hiii