Aliyekuwa bosi wa Kamati ya mashindano wakati Yanga inafika kwa mara ya mwisho hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Hussein Nyika amedai kuwa wanaicheka Simba kutolewa kiutani lakini kuna kitu wanaikumbusha Yanga yao.

Nyika amesema: “Nimeangalia mtani (Simba) hajapoteza nyumbani msimu huu, hii ni rekodi bora sana kwao inayowafanya kulinda hadhi yao. Nilichogundua Simba ni wamoja, hawabaguani inapokuja suala la kulinda heshima ya klabu yao.

“Hapa lazima Yanga wenzangu tujifunze kupitia hili hata kama kafanya Simba, hata wao walijifunza kutoka kwetu katika kutulia na kusajili timu tishio wakiachana na kutumia wachezaji watoto.

nyika

“Ukiangalia mashabiki wa Simba na viongozi wao walikuwa sambamba na wachezaji wao na kuwasaidia kupata mabao yale matatu, Kilichonivutia ni mwisho wa mchezo wote waliwapongeza wachezaji wao, hali ile inamjenga mchezaji kujiona ana thamani ya kuzidi kuipigania timu yake.

“Usajili ni kamari, sawa kuna maeneo unaweza kufanikiwa na usifanikiwe lakini tunatakiwa kuwa makini halitakiwi hili la kusajili kuwa la watu wawili watatu pia wanatakiwa kuwa na fikra za kuangalia jinsi eneo hili lilivyotukwamisha msimu huu.”


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa