Wakati zikiwa zimesalia siku chache dirisha la usajili kufungwa, Man United wanacheza kwa tahadhari kwenye usajili.
Mpaka sasa, Manchester United haijasajili mchezaji yeyote kwenye dirisha hili la januari. Badala yake, kuna uwezekano wakapunguza baadhi ya wachezaji kwa mikataba ya mkopo.
Anthony Martial, Jesse Lingard, Dean Henderson na Donny Van De Beek ni miongoni mwa wachezaji wa United ambao wanauwezekano wa kutoka Old Trafford ndani ya siku chache zilizobaki.
Martial yupo mbioni kujiunga na Sevilla, Lingard anahusishwa na Newcastle, Van De Beek anatajwa sana kule Crystal Palace na Valencia, Henderson bado hakijaeleweka hasa wakati huu ambao Spurs wamemuongezea mkataba Hugo Lloris.
Katika sajili zote hizi, The Red Devils wanatoa wachezaji kwa mikataba ya mkopo bila kipengele cha ulazima/uwezekano wa kumsajili mchezaji husika moja kwa moja ifikapo Juni, 2022. Huu ni mkakati wa tahadhari kwa Manchester kutokana na lengo la uongozi wa timu hiyo kutaka kumpatia kocha mpya atakayekabidhiwa timu, kuamua mchezaji/wachezaji gani abaki nao au anawaeka sokoni.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.