AFCON, raisi wa Caf Patrice Motsepe ametaka uchunguzi wa haraka ufanyike kutokana na janga ambalo lilisababisha vifo vya watu nane na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa, kwenye mchezo wa 16 bora kati ya Cameroon dhidi ya Comoro usiku wa jumatatu.
Taarifa zinasema mashabiki walikuwa wanajaribu kutaka kuingia kwenye kiwanja Paul Biya Stadium, ambacho kina uwezo wa kuingiza watazamaji 60,000, lakini utaratibu mbovu ulisababisha watazamaji kutumia nguvu kutaka kuingia na kusababisha maafa hayo.
Raisi wa Caf Motsepe alijaribua kuangazia baadhi ya makosa yaliosababisha tukio hilo na kwenye mkutano wake na waandishi wa habari alijaribu kuelezea tatizo lililosababisha hayo maafa.
“Baadhi ya watu walikuja kuwa sehemu ya watazamaji, wakiwemo mashabiki wasio na tiketi, nadhani tunakubali kulikuwa na maelfu ya watu kuliko tulivyotarajia, na kwa kusema hivyo, tutakuwa na mazungumzo ya kina, na nina uhakika kwa sababu ya mazungumzo tuliyofanya asubui ya leo.
“Kilichotokea jana ni sababu ya idadi ya watu walioruhusiwa kuingia uwanjani kwa utaratibu uliokuwepo haukuwa umepangiliwa sawasawa na kuongozwa vizuri, na nataraji tukio hilo halitajirudia tena.
“Nilienda kuona watu waliopoteza maisha na kuangalia hiyo sehemu ambayo ilisababisha vifo kwenye sehemu kuingilia, malango ilibidi iwe wazi kwa sababu kama ungekuwa wazi, watu wengeweza kuingia na mlango ukifungwa pasipo sababu inayoeleweka.”
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.