Donny Van De Beek ni miongoni mwa majina yanayopewa nafasi kubwa kwa vijana kule Uholanzi, nchini Uingereza, ni jina la chini kwenye orodha ya wachezaji wa United.
Alisajiliwa kwa £34M akitokea Ajax lakini akiwa anakaribia kutimiza misimu miwili ndani ya Manchester United, Donny Van De Beek hana namba kwenye kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer. Kusugua benchi kumemfanya apoteze namba kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uholanzi chini ya Louis Van Gaal.
Si kweli kuwa, Donny hana kiwango cha kuwazidi baadhi ya wachezaji wanaopewa namba kwenye kikosi cha United. Badala yake, wengi wanamnyooshea kidole Solskjaer kwa kushindwa kuwaongoza wachezaji wake kwa usawa bila upendeleo.

Scot McTominay, Fred, Matic na Paul Pogba wamekuwa wakipewa nafasi kwenye kikosi cha United hata pale wanapoonekana kuwa na viwango vibovu uwanjani. Hii imekua ikiibua maswali mengi kwa Ole na namna yake ya kuongoza kikosi ambacho kinawachezaji wengi wenye uwezo mkubwa kuwazidi hao.
Donny, Juan Mata, Alex Telles, Jesse Lingard na Diogo Dalot ni miongoni mwa wachezaji ambao wanapewa mgongo na Solskjaer kwa sehemu kubwa msimu huu. Pengine mambo yatabadilika kuelekea Januari, 2022.

Paul Pogba ni majeruhi na atakua nje ya uwanja mapaka mwakani. Fred na Scot wanauwezekano mkubwa wa kupumzishwa dhidi ya Watford kutokana na uchovu na kuugua. Hii huenda ikawa ni nafasi kwa Van De Beek kuanza kwenye kikosi cha kwanza wikiendi hii. Muda sindio huu, au Solskjaer atatuambia nini tena katika hili?
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.


