Vilabu vya ligi kuu nchini Uingereza vimekua vikihusishwa na kuinasa saini ya mchezaji Jardon Sancho anaye cheza katika timu ya Borussia Dortmund, mchezeji huyo anaye sakata kabumbu katika nafasi ya kiungo wa pembeni amekuwa na msimu mzuri katika klabu yake ya Dortmund akiwa ameweka kambani goli 17 na kutoa pasi zilizo leta magoli 16 akiwa anashika nafasi ya tatu kwenye ubao wa wafungaji mabao.

Jadon Sancho ambaye ni mzaliwa wa nchi ya Uingereza katika jiji la London amezaliwa mwaka 2000,pia alisha wahi kuvichezea vilabu vya uingereza kama vile Watford na Manchester City.
Sancho alisaini kandarasi yake na Dortmund akitokea Manchester City mwaka 2017, katika msimu wake wa pili tuu aliweza kupangwa katika kikosi cha kwanza na timu hiyo na baadaye kutajwa kwenye kikosi cha msimu katika ligi ya Bundesliga 2018-2019.
Sancho amekwisha shinda taji la DFL SUPER CUP Borussia Dortmund walipo kutana na Bayern Munich
Vilabu vilivyo onesha nia ya kuhitaji huduma ya mchezaji huyo ni timu yake ya zamani Manchester City pia yeye mwenyewe amekua akitamani kurudi klabuni hapo, lakini pia vilabu kama Manchester United, Chelsea na Liverpool vimekua vikimtolea macho kinda huyo anaye washa moto kwelikweli kunako ligi ya Bundesliga

Ingawa mabosi wa Klabu hiyo wamekua wakieleza Sancho ataendelea kubaki klabuni hapo kwa msimu ujao,Sebastian Kehl aliiambia Sky Germany “Tulikua na vitu vichache na Sancho wiki iliyo pita lakini tumesha maliza, Anafanya kazi nzuri sana ana umuhimu kwenye timu yetu alimaliza kwa kusema hivyo.
Thamani ya Jadon Sancho kwa sasa ni zaidi ya yuro milioni 117, akiwa na timu ya Borussia Dortmund pia yupo katiaka kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza akicheza nafasi ya kiungo wa upande wa kulia.


Amani
Sancho tatizo Wana muuza pesa nyingi
Hamidu
Mkali wa assist Sancho njoo man utd utupe raha#meridianbettz
Salma
Madau hatarii
Sadick
Jadon Sancho ni mchezaji mzuri lakini nahisi thamani yake inakuuzwa mno na hizi tetesi za kutakiwa na club kubwa kila mahali#meridianbettz
Lydia Emmanuel Magoti
Sancho tatizo dau kubwa
Povel
Habar njema
Hope mwaikuka
Sancho mtu nomaa
isha
Duuh sancho anauzwa pesa nyingi sana sijajua kwanini au sababu anajua mpira
felister
tatizo asa nini mana hizi tetesi za Sancho zakutakiwa na klabu nyengine nazisikiw takriban kila siku
Gabriel
Sancho bonge la mchezaji anastahil kuuzwa bei juu
Shafii
Naona deal lake linakua ngumu hawaweki mzigo wa kutosha mezani
David Pere
Klabu yenye uwezo wa kumpata Sancho no Man U pere basi
Rehema
Hii ni habari njema
Leonard
Mchezaji mzuri
Agness
Habari nzuri
Neema juma
Chombo kikalii lazima dau lake liongezekee aisee
Theonestina
Ikumbukwe sikuzote ukitaka kizur lazima ughalamie.
Magdalena
Sacho anakubalika kwa kila timu na kuliliwa kwa sababu ya umahili wake
Mwanaidi
Sancho kila klabu inamuhitaji hapo tatizo ni atakayefikia kidau cha kumchukua
Tahiya
Sancho ni mchezaji mzur ila dau lake ni kubwa hasa kipindi iki cha janga la corona vilabu havina mpunga wa kutosha
Furahav
Sancho muda ndo huu wa kula hela.
Kenani
Dogo Yuko vizur Sana juu
warda
Kama Yanga wanavyowinda saini ya Chama#Meridianbettz
Johnmary joel
Jaman kizuri cha jiuza naukitaka vizuri lazima ugaramie mchezaji huyo sancho klabu inayomutaka ijipange#meridianbetz
Emmy cleopa
Habar njema
Genia Sikaluzwe
Sancho fundi wa mpira ndiyo maana wanamwinda
Dorophina
Bado tu hawajapata dau wakakubaliana sancho Ni mchezaji mzuri lazima dau liwe nono
Evaluziga
Sancho tatizo wanamuuza pesa nyingi
lombo
habar njema
Caroline
Sancho kawa mcharo.
Zeiyana
Sancho inapaswa awe na msimamo kama anataka kuondoka au kubaki
Elika
Sancho mchezaji Bora kwangu anastahili kuuzwa kwa gharama yoyote ile
Samiah
Anastahili kuuzwa kwa gharama yyte kwani Sancho nimchezaji bora sanaa
Asia Abdy
Gharama yake sio poa
Khadija
Sancho yupo vzr#meridianbettz
Devotha
Mchezaji mzuri sana ndo maana anagharama kubwa
Ernest
Sancho amekuwa Lulu sana kwenye ulimwengu wa soka